KUWEPO kwa tishio la
Tsunami jana jioni kumepelekea klabu ya soka ya Simba kubadili mpango wao wa
kuingia kambini kujiandaa na mechi zao za Ligi Kuu soka Tanzania
Bara.
Kwa mujibu wa mamapipiro.blogspot Simba ambayo
inatarajiwa kukwaana na Ruvu Shooting jumapili hii kwenye uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam katika mchezo wa ligi hiyo ilitarajiwa kuingia kambini kwenye
hoteli ya Bamba Beach Kigamboni jana jioni.
Ofisa habari wa Simba
Ezekiel Kamwaga alisema baada ya kupata taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa
imebi kutulia kwanza na ndipo watajua mustakabali mzima wa maandalizi ya timu
hiyo ambayo inaiwakilisha Tanzania kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika
(CAF) ikiwa imetinga hatua ya 16 bora ambapo inatarajiwa kukwaana na Al Ahly
Shandy Aprili 22 jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment