![]() |
Ali Ferej Tamim |
RAIS wa chama cha
soka visiwani Zanzibar (ZFA) Ali Ferej Tamim amejiuzulu.
Kwa mujibu wa mamapipiro.blogspot, habari kutoka
visiwani Zanzibar zinasema kwamba Tamim aliyekaa madarakani kwa miaka 20
amewasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa kaimu Katibu Mkuu wa ZFA, Masoud
Attai.
Tamim ameamu kujitoa
katika nafasi hiyo kwa madai ya suala la afya sambamba na kuangalia familia
yake.
Alisema amechua
uamuzi huo bila ya kushinikizwa na yoyote.
Kwa muda mrefu ZFA
chini ya uongozi wa Tamim imekuwa ikilaumiwa kuchangia kuzorota kwa maendeleo ya
soka visiwani humo, huku hali ikionekana kuchafuka hadi kwenye uchaguzi mkuu wa
chama hicho mwaka juzi kutokana na kuwepo kampeni ya kutaka viongozi waliokuwa
madarakani kutaka waendelee kuongoza.
Hata hivyo kamati ya
uchaguzi ilitaka zoezi la uchaguzi lirudiwe mwaka jana ambapo baadhi ya wagombea
walijitoa na mwisho wa siku waliorejea madarakani walikuwa walewale viongozi wa
zamani.
0 comments:
Post a Comment