![]() |
Kanumba |
BARUA iliyotumwa na wawakilishi
watatu wa baba wa marehemu Steven Kanumba, Chales Kanumba, imesomwa jana mbele
ya vyombo vya habari nyumbani kwa marehemu.
Katika barua hiyo baba huyo
alieleza kuwa ameshindwa kufika kwenye msiba baada ya kuugua malaria na
kuandikiwa sindano za masaa.
Barua hiyo iliyotumwa kwa kamati
ya mazishi na ndugu wa familia ilisema: “Salamu katika bwana, kwanza
nawashukuru kwa sana kwa kunitumia usafiri Mungu awe nanyi.”
“Napenda kuwajulisha kuwa tangu
jana (Jumapili), nilikuwa na malaria vidudu 15 na kuandikiwa sindano za masaa,
ilipofika saa 12 asubuhi nikaanza kutapika na kupelekwa hospitali.”
“Nilipofika hospitali nikapimwa
na kukutwa na presha ya kupanda kiwango cha 180 kwa 140 (kawaida 120 kwa 80),
hadi sasa naona kizunguzungu, hivyo nawatuma wawakilishi wangu watatu, Michael
Kanumba, Mbanakheli Kanumba na Clisant Kanumba.”
Pamoja na barua hiyo pia mama
mzazi wa marehemu na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) walitoa shukrani zao
kwa wote waliyohusika kwa namana yoyote.
Mama wa marehemu Steven Kanumba,
Flora Mutegoa, alitoa shukrani zake na kuwaaga waandishi wa habari akisema
anaenda kuliangalia kaburi la mwanae, ambaye alizikwa kwenye makaburi ya
Kinondoni.
Naye Rais wa shirikisho hilo la
filamu Simon Mwakifwamba, alitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wote waliyohusika.
Msanii mwingine aliyeibuliwa na
marehemu Kanumba, Emanuel Myamba, aliwaomba wananchi kutulia na kuachia
mahakama ifanye kazi yake bila kuingiliwa kuhusiana na kifo chake Kanumba.
0 comments:
Post a Comment