![]() |
Berry Black akipagawisha jukwaani |
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya
Mbaraka Abdallah anatarajia kutambulisha wimbo wake mpya uitwao Nyumbani Sio
Safi, Jumapili kwenye Ukumbi wa Club Billicanas.
Berry amesema katika onyesho hilo maalumu kwa ajili ya utambulisho wa wimbo
wake, ataambatana na msanii mwenzake Isihaq Salehe ‘Easy Man’, anayeng’ara na
kibao cha Kasoro Wewe.
“Katika onyesho hilo la Jumapili
nitatambulisha wimbo wangu huo lakini pia nitakuwa na nyingine kibao za
kuwapagawisha mashabiki wangu, nikisindikizwa na swahiba wangu Easy Man,”
alsiema Berry Black.
Berry Black, aliwa kutamba na
kibao cha Nataka Kuwa na Wewe, katoka katika Kundi la 2 Berry akiwa na Berry White.
0 comments:
Post a Comment