Kocha Man Utd Sir Alex Ferguson ajiandaa kwa 'biggest derby'

KOCHA Sir Alex Ferguson amesema kwamba  Manchester United inakabiliwa na mechi ngumu zaidi dhidi ya wapinzani "biggest derby" katika maisha yake yote Old Trafford baada ya kulazimishwa sare ya 4-4 na Everton licha ya kuongoza hadi 4-2 jioni hii.
Wayne Rooney alifunga mabao mawili, lakini mabao ya dakika za mwishoni ya Nikica Jelavic na Steven Pienaar yameibeba Manchester City, ambayo leo imeishusha Wolves kwa kuifunga 2-0.
Kama kikosi cha Roberto Mancini kitaifunga United Jumatatu ijayo, watapanda kileleni kwa tofauti ya mabao, zikiwa zimebaki mechi mbili ligi kufikia tamati.
Ferguson alisema: "Tunahioaji matokeo (mazuri) Uwanja wa Etihad, hakuna swali juu ya hilo."
Alisema: "Tunataka matokeo (mazuri) Uwanja wa Etihad sasa, ni mechi ya upinzani yenye uzito mkubwa - inawezekana mechi muhimu zaidi ya upinzani katika wakati wangu. Lazima twende huko,kuhakikisha tunacheza katika njia nzuri na kutoruhusu nyavu zetu kuguswa.
"Hakuna sababu kwa nini tusipate (matokeo mazuri Etihad). Kumekuwa na matarajio kutoka City kwamba watakuwa waamuzi (wa bingwa), lakini ni uamuzi wetu pia (nani awe bingwa)."