![]() |
Rossi |
KLABU ya Villarreal imesema
mshambuliaji Giuseppe Rossi ameumia tena goti lake la mguu wa kulia na atakuwa
nje ya Uwanja kwa miezi sita zaidi, na kupoteza matumaini ya kuichezea Itali
katika Kombe la Mataifa Ulaya.
Rossi aliumia mguu wake katika
mechi dhidi ya Real Madrid, Oktoba 26 na kufanyiwa upasuaji.
Villarrreal imesema Rossi ameumia
tena mguu wake katika mazoezi leo na anahitaji upasauji mwingine.
Ataukosa mwanzo wa msimu ujao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 25 ameifungia mabao 32 Villarreal katika mashindano yote msimu uliopita.
Raia huyo wa new Jersey, mtoto wa
Wataliano, aliamua kuichezea The Azzurri badala ya Marekani na amefunga mabao
sita katika mechi 27 za kimataifa.
0 comments:
Post a Comment