MABAO ya Sergio Aguero na Samir Nasri yameiiwezesha Manchester City kuishusha Daraja Wolves na kupunguza idadi ya pointi inazozidiwa na vinara wa Ligi Kuu England, Manchester United na kubaki tatu.
Timu zote zilipata nafasi nzuri za kufunga mapema, kabla ya City kupata bao kupitia kwa  Aguero dakika ya 27, akiunganisha krosi safi ya Gael Clichy.
Joe Hart alifanya kazi nzuri kuokoa bao, wakati Steven Fletcher wa Wolves alipopata nafasi nzuri ya kusawazisha, lakini Nasriakafunga la pili dakika ya 74.
Kama City itaifunga United nyumbani Aprili 30, watapanda kileleni zikiwa zimebaki mechi mbili ligi kufikia tamati.