• HABARI MPYA

    Monday, April 16, 2012

    MARADONA: HUYU PELE ANAANZA KUWA CHIZI SASA

    Maradona kushoto, Messi kulia enzi hizo akiwa kocha wa Argnetina
    KOCHA wa Al Wasl ya Dubai, Diego Maradona amemsuta gwiji wa soka Brazil, Pele akimuita mnafiki kwa kusema mshambuliaji wa Santos, Neymar ni bora kuliko nyota wa Barcelona, Lionel Messi.
    Pele alisema Jumanne iliyopita kwamba Messi ni mchezaji babu kubwa, lakini akasema hamfikii nyota huyo wa Santos.
    "Mungu wangu, huo ni upumbavu," alisema Maradona katika taarifa iliyoifikia bongostaz.blogspot.com. "Labda Neymar ni mchezaji bora wa dunia, lakini tu ukisema Messi ni kutoka dunia nyingine."
    Wachezaji wote hao waliingia kwenye tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA, Ballon d'Or Gala, Januari mwaka huu na Messi akashinda tuzo hiyo kama mchezaji bora wa 2011, wakati Neymar akaambulia tuzo ya Puskas, inayotokana na bao bora la mwaka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MARADONA: HUYU PELE ANAANZA KUWA CHIZI SASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top