![]() |
Van Persie |
![]() |
Rooney na Wellbeck |
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Robin van Persie ni miongoni mwa
wachezaji sita walioingizwa kwenye kinyang’anyiro cha Chama cha Wachezaji wa
Kulipwa England, PFA katika Ligi Kuu msimu.
Nahodha huyo Arsenal amekuwa na msimu mzuri akifunga mabao
ya kutosha, hadi sasa akiwa ametikisa nyavu mara 27 katika ligi na kutoa pasi
za mabao 10 kwa wachezaji wenzake.Alex Oxlade-Chamberlain, wakati huo huo ameingizwa kwenye kipengele cha kuwania tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka.
Mshindi wa tuzo hizo anatarajiwa kutajwa Jumapili.
Orodha ya wanaowania tuzo Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA: Robin van Persie (Arsenal), Wayne Rooney (Manchester United), Scott Parker (Tottenham), Sergio Aguero, Joe Hart, David Silva (wote Manchester City).
Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka PFA: Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Gareth Bale, Kyle Walker (both Tottenham), Danny Welbeck (Manchester United), Sergio Aguero (Manchester City), Daniel Sturridge (Chelsea).
0 comments:
Post a Comment