• HABARI MPYA

    Friday, April 13, 2012

    XAVI ANASEMA MESSI ATAFUNIKA WOTE PELE NA MARADONA


    Xavi anaamini kwamba mchezaji mwenzake wa Barcelona, Lionel Messi anaelekewa kuwa mwanasoka bora daima katika historia ya soka.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Argentina, ameshinda Ballon d'Or kwa miaka mitatu mfululizo iliyopita na hivi karibuni ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa klabu yake akiwa ana umri wa miaka 24.
    Xavi anaamini kwamba Messi anaelekea kuwapiku magwiji wa dunia kama Pele na Diego Maradona.
    "Kama ataendelea hivyo, kasha nafikiri Messi atakuwa mchezaji bora katika historia ya soka," nyota huyo wa kimataifa wa Hispania, aliiambia FIFA.com.
    Xavi amesema amebarikiwa kuwa kwenye kikosi hiki cha Barcelona ambacho kinapewa heshima ya kikosi bora zaidi ambacho hakijawahi kuonekana katika mchezo huo.
    Pamoja na hayo, amesema kwamba kuna magwiji wachache angependa kucheza nao.
    "Ningependa kucheza na [Zinedine] Zidane na Ronaldo. Lakini nimekuwa mwenye bahati ya kutoshan kucheza Barcelona na timu ya taifa, hivyo nimefanya kazi na wachezaji wengi wazuri pamoja na watu babu kubwa na makocha ambao wamenifundisha vizuri," Xavi alisema.
    "Wakati wote unataka kucheza nyota wakubwa na watu babu kubwa katika ulimwengu wa soka.
    "Ningependa kufundishwa na [Johan] Cruyff kuona anafanyaje kazi, kwa sababu nimesikia mambo mengi mazuri," alisema.
    Xavi ni kipaji kilichoibuliwa na timu ya vijana ya Barca, na sasa yupo karibuni kutimiza mechi 700 kwenye michuano yote katika klabu hiyo ya Catalan
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: XAVI ANASEMA MESSI ATAFUNIKA WOTE PELE NA MARADONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top