![]() |
| Lino Masombo kushoto, akimpongeza Juma Kaseja baada ya fainali ya Kombe la Urafiki, ambayo Simba iliifunga Azam FC kwa penalti, baada ya sare ya 2-2. |
Na Mahmoud Zubeiry
1.
Kwa nini habari zilivuja Mwenyekiti wa Simba SC
alimpa Mbuyu Twite dola za Kimarekani 30,000, wakati sasa inaelezwa mchezaji
huyo alipewa dola 10,000 tu
2.
Simba ilisema ilimuongezea mkataba Kevin Yondan,
je ilimpa na fedha? Na kama ilimpa fedha mbona hazijavuja habari zozote juu ya
fedha alizopewa, wakati inajulikana hadi Felix Sunzu analipwa dola za
Kimarekani 3,500 kwa mwezi?
3.
Simba ilimsajili na kumpa fedha beki Lino
Masombo kutoka DRC, tena inaelezwa ni fedha nyingi tu, je baada ya kumtema bila
kumpa muda wa kutosha kujiridhisha kuhusu uwezo wake (mdogo au mkubwa), ili
kukwepa kurudia makosa yaliyofanyika katika kumtema Derrick Walullya, fedha
hizo zinarudishwa au?
4.
Ukitazama kikosi cha Simba kwa sasa utagundua
wamesheheni viungo kibao, Amri Kiemba, Jonas Mkude, Christopher Edward, Mussa
Mudde, Haruna Moshi, Kanu Mbivayanga, Mwinyi Kazimoto, Uhuru Suleiman, Kiggi
Makassy, Salim Kinje, Ramadhan Singano ‘Messi’, Mrisho Ngassa na Ramadhan
Chombo ‘Redondo’, wakati mabeki wa kati ni Juma Nyosso, Shomary Kapombe na Obadia
Mungusa, (Zingatia, kiasili Kapombe na Maftah kiasili ni viungo) je, hii iko
sawa?
5.
Nani huwa anashauri masuala ya usajili ndani ya Simba…Kusajiliwa
au kukatwa kwa mchezaji, je anafanya kazi yake vizuri?
6.
Kitaalamu inafahamika, kumchezesha mchezaji mechi,
kabla hajawa fiti kwa angalau zaidi ya asilimia 50 ni kumtengenezea mazingira
ya kuumia na tumeshuhudia majeruhi wengi katika siku za karibuni Simba SC, je
kwa nini Kocha Mkuu, Mserbia Milovan Cirkovick anaruhusu hali hii?
![]() |
| NANI MSHAURI WAO; Benchi la Ufundi Simba SC kutoka kushoto Kocha Mkuu, Milovan Cirkovick (Serbia), Msaidizi Hamatre Rochard (Uganda) na Kocha wa makipa, Mzalendo, James Kisaka. |




.png)
0 comments:
Post a Comment