• HABARI MPYA

    Thursday, August 09, 2012

    NGORONGORO WAWAFUATA EAGLES BILA ULIMWENGU, NDITI

    Wachezaji wa Ngorongoro
    Na Princess Asia
    TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imeondoka leo Dar es Salaam kwenda Nigeria kwa ajili ya mechi ya marudiano na Flying Eagles kuwania kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo, zitakazofanyika nchini Algeria mwakani.
    Katika mchezo huo utakaochezwa Jumapili, Ngorongoro inahitaji kushinda 2-0 ili kusonga mbele, baada ya awali kufungwa na Nigeria mabao 2-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki iliyopita, mabao ya mshambuliaji wa Enugu Rangers, Achaji Gero katika dakika ya pili na 44.
    Bao la Ngorongoro lililofungwa na mshambuliaji mpya wa Coastal Union ya Tanga, Atupele Green aliyesajiliwa kutoka Yanga B, dakika ya 50, akimalizia krosi ya Ramadhani Singano ‘Messi’.
    Ngorongoro wangeweza kupata mabao zaidi kwenye mechi hiyo, kama wangecheza soka ya chini, lakini kutia krosi za juu kwenye lango la Nigeria ilikuwa ni kuwatesa washambuliaji wao wafupi, Atupele na Simon Msuva.
    Baada ya mchezo huo, kocha wa Ngorongoro Heroes, Mdenmark Jakob Michelsen alisema kwamba ataongeza nguvu katika kikosi chake kwa kuwaita wachezaji wawili wanaocheza nje, kiungo Adam Nditi wa Chelsea na Thomas Ulimwengu wa Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), sambamba na nyota wengine waliokwenda Ujerumani n TSU kwenye michuano ya Fallerhof.
    Bahati mbaya kwake, siyo tu Chelsea haijamruhusu Nditi, bali hata Mazembe, safari hii imegoma kumpandisha ndege Ulimwengu.
    Katika mchezo wa kwanza, vikosi vilikuwa; Ngorongoro; Barwany Khomein, Omega Seme, Jamal Mroki, Issa Rashid, Ruhana Samir, Yarouk Ramadhan, Kheri Salum/Jerome Lambele, Frank Damayo, Simon Msuva, Atupele Green na Ramadhan Singano.
    Flying Eagles; Samuel Okani, Hassan Abubakar, Ahiyu Mohamed, Ikechukwu Okine, Chizoba Amaefule, Agboyi Oubokha, Moses Orkuma, Chidi Osochukwu, Yahaya Adam/Harrison Egbune, Achaji Gero na Aminu Omar/Uchw Agbo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGORONGORO WAWAFUATA EAGLES BILA ULIMWENGU, NDITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top