![]() |
Mzee Gurumo, mkongwe wa Msondo |
Na Prince Akbar
Bendi zenye upinzani wa jadi nchini kama ule wa Simba na
Yanga, Msondo Ngoma Music Band na
Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae) zitapambana siku ya Iddi Mosi kwenye viwanja
vya Leaders Club, Kinondoni.
Tayari mashabiki wa bendi hizo wameanza maandalizi ya
kuzishangilia bendi zao.
Mpambano huo umeandaliwa na kampuni za Keen Arts na
kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo
litakuwa la kusherekea sikukuu ya Iddi na kuamua ni bendi gani bora kati ya
magwiji hao wawili wa muziki wa dansi nchini kwa mwaka 2012.
Kapinga alisema ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa, kila
bendi itatumia jukwaa lake kwa kupiga kwa muda wa saa moja kabla ya nyingine
kupanda jukwani.
“Litakuwa pamabano la aina yake ukizingatia kuwa itakuwa ni
mara ya kwanza kwa bendi hizi pinzani kupambana siku ya sikukuu ya Iddi tangu
zianzishwe” alisema Kapinga.
“Pia itakuwa ni mara ya kwanza kwao kushindana katika
viwanja vya Leaders Club.”
Kapinga alisema kampuni yake inafanya mipango ya
kuwasafirisha wapenzi wa bendi hizo kutoka kila wilaya ya Dar es Salaam kuja
kushuhudia mpambano huo.
Alisema mchuano huo itaanza saa nane mchana hadi liamba.
Mwaka jana bendi hizo zilipambana vikali kwenye ukumbi wa
TCC Club sikukuu ya Krismasi ambapo mbali na muziki safi na vituko vya hapa na
pale kama ilivyo kawaida, zilitoka sare kwa kupata pointi sawa.
Mratibu amesema kuwa mwaka huu mshindi ni lazima apatikane
hata kwa kurusha shilingi.
0 comments:
Post a Comment