 |
Juma Kaseja mazoezini |
 |
John Bocco kulia, nyuma yake ni kocha Poulsen |
 |
Bocco kulia na Poulsen |
 |
Bahanuzi na Boban kulia |
 |
Ngassa na Bahanuzi kulia |
 |
Bocco na Boban kujia |
 |
Ngassa na Nyoni |
 |
Kocha wa makipa Juma Pondamali kulia, akiwaongoza makipa Kaseja, Dida na Mwadini |
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo imeanza maandalizi
ya mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana utakaochezwa Jumatano
ijayo mjini Gaborone.
BIN ZUBEIRY ilitembelea Uwanja wa Karume jioni ya leo, na kuwakuta
wachezaji wa timu hiyo wakijifua chini ya walimu wao, Mdenmark Kim Poulsen na
wasaidizi wake Sylvester Marsh na Juma Pondamali.
Wachezaji waliokuwapo mazoezini ni makipa Deogratias Munishi
(Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha
msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na
Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna
Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo
(Azam), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi
(Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP
Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon
Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-
DRC).
Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, itaondoka Dar es Salaam Jumanne.
0 comments:
Post a Comment