Na Ally Mohamed,
Zanzibar
TIMU ya Bandari
imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Mafunzo katika Ligi Kuu ya Zanzibar leo
kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Bandari
walikuwa wa kwanza kuliona lango la Mafunzo kupitia mshambuliaji wao Mussa Omar
'Kidishi' katika dakika ya 25 na Mafunzo walisawazisha kupitia kwa Mohammed
Abdulrahim dakika ya 52.
Kwenye Uwanja
wa Gombani, Pemba, Jamhuri ambao ni wawakilishi wa Zanzibar katika Kombe la Shirikisho
mwakani, wametandikwa na Chipukizi mabao 3-0. Mabao ya Chipukizi yalifungwa na
Muhsin Mohammed dakika ya 11, Faki Maalim dakika ya 21 na 60.
Ligi hiyo
inatarajia kuendelea tena kesho kwa mechi moja Uwanja wa Amaan kwa kuzikutanisha
timu za Mtende Rangers na Chuoni.



.png)
0 comments:
Post a Comment