Tetesi za J'mosi magazeti Ulaya
MAN CITY, CHELSEA ZAKABANA KOO KUWANIA SAINI YA OLIVIEIRA
Chelsea na Manchester City zinaongoza katika mbio za kumuwania mshambuliaji mmoja hatari sana Ulaya anayechezea Benfica ya Ureno, Nelson Oliveira, mwenye umri wa miaka 20 ambaye thamani yake ni pauni Milioni 24.
Manchester City inatumai kutumia maarifa ya Ofisa wake Mtendaji Mkuu mpya, Ferran Soriano wa Barcelona kuwanasa mshambuliaji wa thamani ya juu, Cristian Tello, mwenye umri wa miaka 21, kiung Sergi Roberto, mwenye miaka 20 na winga Gerard Deulofeu, mwenye miaka 18.
Emile Heskey - ambaye yuko huru tangu aondoke Aston Villa mwishoni mwa msimu uliopita, anatakiwa na timu ya Ligi ya Conference, Macclesfield ambayo inaamini mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na England mwenye umri wa miaka 34, atawarejesha kwenye Ligi za Soka England.
Fulham inamtaka kipa wa Standard Liege, Sinan Bolat, mwenye umri wa miaka 24, akazibe nafasi ya Mark Schwarzer.
Kiungo David Meyler, mwenye umri wa miaka 23, atabaki Sunderland baada ya kocha Martin O'Neill kughairi kumtoa kwa mkopo Hull.
QPR HAITAMSHURTISHA FERDINAND KUMPA MKONO JT
QPR haitamuamrisha beki Anton Ferdinand kupeana mikono na wachezaji wa Chelsea, licha ya Bodi ya Ligi Kuu kuamua kwamba kanuni za kabla ya mechi zinabaki kama zilivyo. Ferdinand, mwenye umri wa miaka 27, ameamua kutofuata itifaki hiyo kwa John Terry, mwenye umri wa miaka 31, au Ashley Cole, mwenye umri kama huo pia, katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya Chelsea, tangu Nahodha huyo wa The Blues, Terry asafishwe na Mahakama kwa kashfa ya ubaguzi dhidi yake.
Mshambuliaji wa Aston Villa, Darren Bent, mwenye umri wa miaka 28, amesema kwamba hataki kupuuzia msimu huu, na atathibitisha anastahili kuendelea kuwamo kwenye kikosi cha England katika zama mpya za kocha Roy Hodgson.
Winga Mnigeria wa Chelsea, Victor Moses alikuwa ana umri wa miaka 11 wakati wazazi wake wanauawa katika mapambano ya kidini; "Popote walipo kwa sasa, lazima wajivunie mimi, wanaangalia chini wakijivunia mimi."
Kocha wa zamani wa Everton, Howard Kendall amemuonya Marouane Fellaini, mwenye umri wa miaka 24, kuchunga mdomo wake baada ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, kusema ataondoka Goodison Park Januari.


.png)
0 comments:
Post a Comment