• HABARI MPYA

    Saturday, September 15, 2012

    SAMATTA, ULIMWENGU KATIKA SHUGHULI MUHIMU NA NZITO AFRIKA KESHO

    Mbwana Ally Samatta ataiongoza TP Mazembe dhidi ya Berekum Chelsea nchini Ghana kesho, je ataendeleza kutikisa nyavu Afrika? 

    Na Mahmoud Zubeiry
    HATUA ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, inatarajiwa kukamilika kesho kwa mechi nne za makundi yote, A na B kupigwa kwenye viwanja vine tofauti, kutafuta timu nne za kuingia Nusu Fainali.
    Katika Kundi A, ASO Chlef watakuwa wenyeji wa Esperance ya Tunisia na Sunshine Stars wataikaribisha Etoile du Sahel ya Tunisia pia, wakati Kundi B, Berekum Chelsea ya Ghana itakuwa mwenyeji  wa TP Mazembe ya DRC, yenye washambuliaji wawili wa Kitanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu na wapinzani wa jadi wa soka ya Misri, Al Ahly na Zamalek watamenyana mjini Cairo.
    Mechi zote za kukamilisha hatua hiyo, zitachezwa Saa 12:00 jioni zikianza na kumalizika muda mmoja ili kukwepa kupanga matokeo.
    Katika Kundi A, Esperance inaongoza kwa pointi zake 13, baada ya kucheza mechi tano, ikifuatiwa na Sunshine Stars yenye pointi saba, wakati ES Sahel ina pointi tano katika nafasi ya tatu na ASO Chlef haina pa kwenda ikiwa mkiani na haina pointi hata moja.
    Kundi B ndio kuna kazi, TP Mazembe na Al Ahly tayari zote zimevuna pointi 10 kila moja ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine katika kundi lao, maana yake zimekwishafuzu Nusu Fainali, tofauti na Kundi A, ambako Sunshine Stars na ES Sahel zinawania kuungana na Esperance ambayo haing’oleki tena kileleni.
    Lakini pia Kundi B, Ahly na Mazembe inayoongoza kwa wastani wa bao moja zaidi, zote zitapigania ushindi mnono ili kukwepa nafasi ya pili zisikutane na Esperance ya Tunisia katika Nusu Fainali, kwani nayo inatisha. Zote zinaamini bora kukutana na Esperance Fainali.
    Lakini hata timu ambazo hazina nafasi hazitalegea, kwa sababu zinapofanya vizuri zinajiongezea bonasi kutoka kwenye mashindano, hivyo mechi zote zinatarajiwa kuwa ngumu leo kwa sababu hata sare, au kila bao ni fedha.  

    MSIMAMO WA MAKUNDI:
    KUNDI A
                                     P    W  D   L    GF GA GD Pts
    1    Esperance           5    4    1    0    7    2    5    13
    2    Sunshine Stars    5    2    1    2    4    4    0    7
    3    ES Sahel             4    1    2    1    1    1    0    5
    4    ASO Chlef           4    0    0    4    3    8    -5  0

    KUNDI B
                                          P    W  D   L    GF GA GD Pts
    1    TP Mazembe            5    3    1    1    9    5    4    10
    2    Al Ahly                      5    3    1    1    8    5    3    10
    3    Berekum Chelsea     5    1    3    1    8    10 -2  6
    4    Zamalek                   5    0    1    4    4    9    -5  1

    RATIBA NA MUDA WA MECHI ZA KESHO:
    ASO Chlef                v    Esperance           (Saa 12:00 jioni) 
    Sunshine Stars         v    ES Sahel             (Saa 12:00 jioni) 
    Berekum Chelsea     v    TP Mazembe       (Saa 12:00 jioni) 
    Al Ahly                      v    Zamalek              (Saa 12:00 jioni)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA, ULIMWENGU KATIKA SHUGHULI MUHIMU NA NZITO AFRIKA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top