Tetesi za Jumapili magazeti Ulaya


MAN UNITED BADO INAYE TU FELLAINI, CHELSEA WATENGA PAUNI MILIONI 30


Manchester United bado inamfuatilia Marouane Fellaini wa Everton baada ya kiungo huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24, kunukuliwa akisema atakaa kwa msimu mmoja zaidi Goodison.
Pamoja na hayo, Chelsea nayo inataka kuipa Everton pauni Milioni 30 kwa ajili ya Fellaini.
Joao Moutinho
Joao Moutinho: Spurs wakipanda dau wanaweza kumsajili tena.
Kiungo wa Liverpool, Jonjo Shelvey, mwenye umri wa miaka 20, amesema wachezaji wa klabu hiyo walistaajabu mno kuona hakununuliwa mchezaji yeyote kuziba pengo la Andy Carroll kabla ya kufungwa kwa pazia la usajili.
Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy hakutaka kutoa dau la pauni Milioni 24 kumununua kiungo wa Porto, Joao Moutinho kabla ya kufungwa kwa pazia la usajili.
Beki wa Stockport County, Kyle Brownhill, 17, anafuatiliwa na klabu za Wigan, Blackburn Rovers, Leeds United na Nottingham Forest.

DROGBA ALISHINDWA KUTEMBEA

Didier Drogba amesema alishindwa kutembea baada ya klabu yake ya zamani, Chelsea kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa penalti Mei, mwaka huu.
Manchester City are poised to announce that they have reduced their losses by £60m compared with last year.
Anton Ferdinand anafikiria kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya John Terry ikiwa beki huyo wa Chelsea hatapewa adhabu kali na FA kwa tuhuma za ubaguzi dhidi yake.
Nahodha wa Reading, Jobi McAnuff, mwenye umri wa miaka 30, amesema mishahara mikubwa wanayopewa wachezaji katika Ligi Kuu ya England ianachangia kuharibu mhezo huo.