![]() |
Kocha Tom |
![]() |
Kocha wa Mtibwa, Mecky Mexime |
![]() |
Kocha Tom |
![]() |
Mashabiki wa Yanga |
![]() |
Mashabiki wa Yanga |
![]() |
Mashabiki wa Yanga mwanzoni mwa mchezo kabla hawajafungwa |
![]() |
Waandishi wa Habari kazini |
![]() |
Hatari langoni mwa Mtibwa |
![]() |
Simon Msuva chini ya ulinzi mkali |
Na Mahmoud Zubeiry,
Morogoro
BAADA ya
kuchapwa mabao 3-0 leo na wenyeji Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro kwenye
Uwanja wa Jamhuri mjini hapa, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, Yanga walipata wakati mgumu kutoka uwanjani kutokana na hasira za
mashabiki.
Mpira ulipoisha
mashabiki wenye hasira walivamia uwanjani na kulizingira basi la wachezaji,
kabla ya askari Polisi kujitokeza kuwatawanya, hatimaye kufanikiwa kuondoka
baada ya takriban nusu saa tangu mchezo umalizike.
Kwa ujumla,
mashabiki wa Yanga waliohudhuria mechi hiyo wamesononeshwa mno na kiwango cha
chini kilichoonyeshwa na wachezaji na timu kwa ujumla katika mchezo wa leo.
Maswali mengi
yanaibuka- kulikoni timu imeshuka kiwango ghafla, wakati ilikuwa moto wa kuotea
mbali siku chache zilizopita hadi kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame.
Hofu imekwishaanza
kutawala kwa baadhi ya wana Yanga, labda kilichotokea katika msimu uliopita,
Yanga kutoka kutwaa Kombe la Kagame na kushindwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu,
tena ikifungwa 5-0 na wapinzani wao wa jadi, Simba kinaweza kujirudia na msimu
huu.
Na kwa
kuzingatia wapinzani wao wa jadi, Simba leo wameshinda mechi ya pili ya Ligi
Kuu, mabao 2-0 dhidi ya timu ngumu, JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
tena wakiwa pungufu baada ya Emanuel Okwi kutolewa kwa kadi nyekundu, wasiwasi
unazidi Yanga.
Katika mchezo
wa leo, Yanga ilizidiwa mno na hadi mapumziko, tayari Mtibwa Sugar walikuwa
mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na beki wa kati, Dickson Daudi dakika
ya 11 akiunganisha kwa kichwa kona ya beki wa kushoto Malika Ndeule.
Bao hilo
lilitokana na uzembe wa mabeki wa Yanga ambao walishindwa kumuweka ulinzi
mchezaji mrefu kuliko wote, Daudi.
Yanga
walijaribu kutaka kusawazisha, lakini mipango yao haikuwa na tija na kujikuta
wakiendelea kushambuliwa na dakika ya 43, Hussein Javu aliwainua tena vitini
mashabiki wa Simba waliokuwa wakiwashangilia kwa nguvu leo kwa kufunga bao la
pili.
Kwa ujumla
kipindi cha kwanza, Yanga walicheza ovyo- pasi zao nyingi zilikuwa hazifiki,
walishindwa kuwabana wapinzani wao na zaidi Haruna Niyonzima alishindwa
kuiongoza vema timu, jambo ambalo lilifamnya kiungo mkabaji Athumani Iddi
‘Chuji’ kupanda mbele zaidi kusaidia, ingawa haikusaidia.
Mabeki
wawili wa kati wa Mtibwa, Daudi na Salvatory Ntebe waliwadhibiti vema washambuliaji
wawili wa Yanga, Hamisi Kiiza na Saidi Bahamnuzi katika dakika 45 za kipindi
cha kwanza.
Kipindi cha
pili, Kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet alianza kwa mabadiliko akiwatoa
Frank Damayo na David Luhende na kuwaingiza Simon Msuva na Stefano na Mwasyika,
lakini bado ukuta wa Mtibwa ulikuwa mgumu mbele ya Watoto wa Jangwani.
Katika
kuongeza mashambulizi, Mtakatifu Tom alimtoa beki Mbuyu Twite na kumuingiza na
mshambuliaji Didier Kavumbangu, lakini bado mambo yaliendelea kuwa magumu kwa
Yanga.
Dakika ya 86
Hussein Javu aliifungia Mtibwa bao la tatu kwa shuti la mbali, wakitoka
kushambuliwa na kufikia hapo, Yanga ‘walikufa’ na mashabiki wao wakaanza
kuuacha Uwanja wa Jamhuri.
Huu unakuwa
mchezo wa pili kwa Yanga tangu kuanza kwa ligi wakiwasononesha mashabiki wao,
baada ya mechi ya kwanza kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye
Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Waswahili
wanasema siku ya kufa nyani, miti yote huteleza, Hamisi Kiiza alipaisha mkwaju
wa penalti dakika ya 89, baada ya Daudi kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, ,
Mbuyu Twite/Kavumbangu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi
‘Chuji’, Frank Domayo/Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi
Kiiza na David Luhende/Stefano Mwasyika.
Mtibwa Sugar; Shaaban Hassan Kado, Malika Ndeule, Issa
R Issa, Dickson Daudi, Salvatory Ntebe, Shaaban Nditi, Jamal Mnyate/Babu Ally
Seif, Awadh Juma, Hussein Javu, Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Vincent Barnabas/Ally
Mohamed ‘Gaucho’.
Katika mechi
nyingine, Simba SC imeendeleza wimbi la
ushindi, baada ya kuichapa JKT Ruvu mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
licha ya kucheza pungufu baada ya Emanuel Okwi kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Mabao ya Simba yalitiwa kimiani na
viungo Amri Kiemba na Haruna Moshi ‘Boban’ na kwa matokeo hayo, Simba
inaendelea kuongoza ligi kwa kufikisha pointi sita, baada ya awali kuifunga
African Lyon 3-0.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’,
Amir Maftah, Shomary Kapombe, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna
Moshi ‘Boban’, Daniel Akuffo, Mrisho Ngassa na Emanuel Okwi.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Uwanja
wa CCM Kirumba mjini Mwanza Azam imelazimishwa sare ya 2-2 na wenyeji Toto African, Uwanja
wa Kaitaba Bukoba, wenyeji Kagera Sugar wametoka sare ya bila kufunga na JKT
Oljoro ya Arusha, wakati Uwanja wa Sokoine Mbeya, wenyeji Prisons wametoka sare
ya 1-1 na Coastal Union ya Tanga na kwenye Uwanja wa Chamazi, African Lyon
imeifunga Polisi Morogoro 1-0, wakati Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Ruvu
Shooting imeifunga 2-1 Mgambo JKT.
MSIMAMO WA LIGI KUU BARA
P W D L GF GA GD P
Simba SC 2 2 - - 5 - 5 6
Mtibwa Sugar 2 1 1 - 3 - 3 4
Azam FC 2 1 1 - 2 1 1 4
Coastal 2 1 1 - 2 1 1 4
Ruvu
Shooting 2 1 - 1 3 3 - 3
JKT Ruvu 2 1 - 1 2 3 -1 3
African Lyon 2 1 - 1 1 3 -2 3
Toto African 2 - 2 1 3 2 1 2
JKT Oljoro 2 - 2 1 1 - - 2
Prisons 2 - 2 - 1 1 - 2
Polisi Moro 2 - 1 1 - 1 -1 1
Kagera Sugar 2 - 1 1 - 1 -1 1
Yanga SC 2 - 1 1 - 3 -3 1
JKT Mgambo 2 - - 2 1 3 -2 0
MATOKEO MECHI ZOTE LEO:
JKT Ruvu 0-2
Simba SC
Mtibwa Sugar
3-0 Yanga SC
African Lyon
1-0 Polisi Moro
Ruvu
Shooting 2-1 Mgambo JKT
Prisons 1-1
Coastal Union
Kagera Sugar
0-0 JKT Oljoro
Toto
Africans 2-2 Azam FC
MECHI
ZIJAZO;
Septemba 22, 2012
Yanga SC Vs
JKT Ruvu (Taifa, Dar es Salaam)
Azam FC Vs
Mtibwa Sugar (Chamazi, Dar es Salaam)
JKT Oljoro
Vs Polisi Morogoro (Amri Abeid, Arusha)
Coastal
Union Vs Toto Africans (Mkwakwani, Tanga)
Septemba 23, 2012
Mgambo JKT
Vs Kagera Sugar (Mkwakwani, Tanga)
Simba SC Vs
Ruvu Shooting (Taifa, Dar es Salaam)
African Lyon
Vs Prisons (Chamazi, Dar es Salaam)
0 comments:
Post a Comment