SIMBA SC imeendeleza wimbi la ushindi
katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanania Bara, baada ya kuichapa JKT Ruvu mabao 2-0 Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam, licha ya kucheza pungufu baada ya Emanuel Okwi
kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Mabao ya Simba yalitiwa kimiani na
viungo Amri Kiemba na Haruna Moshi ‘Boban’ na kwa matokeo hayo, Simba
inaendelea kuongoza ligi kwa kufikisha pointi sita, baada ya awali kuifunga
African Lyon 3-0.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’,
Amir Maftah, Shomary Kapombe, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna
Moshi ‘Boban’, Daniel Akuffo, Mrisho Ngassa na Emanuel Okwi.
Katika
mechi nyingine za ligi hiyo, Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Azam
imelazimishwa sare ya 2-2 na wenyeji Toto African, Uwanja wa Kaitaba
Bukoba, wenyeji Kagera Sugar wametoka sare ya bila kufunga na JKT Oljoro ya
Arusha, wakati Uwanja wa Sokoine Mbeya, wenyeji Prisons wametoka sare ya 1-1 na
Coastal Union ya Tanga na kwenye Uwanja wa Chamazi, African Lyon imeifunga Polisi
Morogoro 1-0, wakati Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Ruvu Shooting imeifunga 2-1 Mgambo.![]() |
Emanuel Okwi akishangaa baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu |
0 comments:
Post a Comment