Tetesi za Jumanne magazeti Ulaya
MKURUGENZI ALITAKA CHELSEA ARUDISHWE LIVERPOOL
Mkurugenzi wa zamani wa Michezo wa Chelsea, Damien Comolli alitaka Chelsea imrejeshe mshambuliaji Fernando Torres, mwenye umri wa miaka 28, katika klabu ya Liverpool.
Manchester United imepanga kupambana na Chelsea na Manchester City katika kuwania saini ya nyota wa Ureno, Nelson Oliveira. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, amefunga mabao mawili katika La Liga tangu apelekwe kwa mkopo Deportivo la Coruna kutoka Benfica.
Beki wa kushoto wa Sunderland, Danny Rose, mwenye umri wa miaka 22, anatumai kuugeuza mkataba wa mkopo Tottenham Hotspur kuwa wa kudumu.
Kocha wa West Ham, Sam Allardyce ameamua kutowasaini mabeki Mikael Silvestre, mwenye umri wa miaka 35, na Anthony Vanden Borre, mwenye miaka 24, kama wachezaji huru.
Klabu za Daraja la Kwanza, Leeds United na Leicester City zinamgombea mshambuliaji wa Stoke City, Kenwyne Jones, mwenye umri wa miaka 27, kwa mkopo.
FA YAMTARAJIA HARAKA ASHWORTH
Chama cha Soka kinatumai Dan Ashworth, Mkurugenzi mpya wa mradi wa maendeleo, atakuwa kazini Uwanja wa St George Park kabla ya msimu ujao. Mtaalamu huyo mwenye umri wa miaka 41 kwa sasa anautumikia mkataba wake wa miezi 12 katika klabu ya West Bromwich Albion, ambao unamalizika Juni mwaka huu, lakini FA wapo kwenye majadiliano kuangalia namna ya kuvunja mkataba huo.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema mustakabali wa mkataba wa Theo Walcott kutoeleweka unaweza kuchangian hata yeye kutomteua katika kikosi cha kwanza. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu ujao na tayari amekataa mshahara wa pauni 75,000 kwa wiki kuongeza.
Manchester United inatarajiwa kutoa ripoti ya kushuka kwa mapato na faida zao za msimu leo, hayo yakiwa matokeo ya timu hiyo kushindwa kufanya vizuri msimu uliopita kwenye Ligi ya Mabingwa.
Kipa Anders Lindegaard, mwenye umri wa miaka 28, anaamini klabu yao ya Old Trafford itavuka kutoka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Paul Ince, Mark Robins, Phil Brown na Richard Money wote wapo katika nafasi ya kuupata ukocha wa Coventry City.
Nahodha John Terry, mwenye umri wa miaka 31, anatarajiwa kuwa fiti kwa mechi nya kesho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Chelsea ikifungua dimba na vinara wa Italia, Juventus baada ya jana kufanya mazoezi.
Kukosa washambuliaji kumemfanya kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers kumuita kinda Samed Yesil, mwenye umri wa miaka 18, katika kikosi chake cha mechi ya Europa League dhidi ya Young Boys keshokutwa, licha ya awali kusema mchezaji huyo angehitaji mwaka mmoja au miwili kabla ya kuanza kupewa nafasi.
0 comments:
Post a Comment