![]() |
Mtakatifu Tom akiwaongoza vijana wake |
Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA Mkuu
wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet amewaomba radhi mashabiki wa Yanga kwa sare ya
Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine na amesema kesho anapeleka wachezaji 18
Morogoro kwa ajili ya mechi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi
ya Mtibwa Sugar, akiwa ana matumaini makubwa ya ushindi.
Saintfiet ameiambia
BIN
ZUBEIRY leo kwamba sababu nyingi zilichangia Yanga kutocheza kwa ubora
wake Mbeya, ikiwemo hoteli mbaya na chakula kibaya na kwa ujumla alisema
hawakuwa vizuri kabla ya mechi hiyo.
“Mimi kwa
mfano sijaoga siku mbili, kwa kweli tulikuwa katika mazingira magumu na
wapinzani wetu walicheza soka ya kuudhi tangu mwanzo, kupoteza muda, na marefa
hawakuchukua hatua, tulipoteza nafasi kupitia kwa Kiiza (Hamisi) na Msuva (Simon),
siwezi kulaumu mchezaji wangu yeyote, lakini hiyo ndiyo hali halisi,”alisema
Saintfiet.
Alisema kesho
asubuhi timu itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar
es Salaam na saa 8:00 mchana watasafiri kwa njia ya barabaraba kwenda Morogoro
ambako wakifika watatafuta hoteli nzuri mapema.
Alisema anajua
hata Uwanja wa huko, Jamhuri si mzuri na mechi itakuwa ngumu kwa sababu Mtibwa
Sugar nao walitoka sare ya bila kufungana na Polisi katika mchezo wao wa kwanza
Jumamosi na anaiheshimu timu hiyo kama moja ya timu tano kubwa Tanzania, pamoja
na Simba, Azam na Coastal Union.
“Lakini
pamoja na kwamba Simba wamependelewa kupangiwa ratiba ya kuanza kucheza
nyumbani mechi tano mfululiuzo, nakuambia Mei mwaka 2013 Yanga ndio itavishwa
taji la ubingwa wa Ligi Kuu, acha wafurahie sasa hivi, watalia mwisho,”alisema
Mtakatifu Tom.
Kuhusu wachezaji
18 anaokwenda nao Morogoro, Mtakatifu Tom alisema atawataja baada ya mazoezi ya
kesho na hiyo inaonekana ni kwa sababu ya kufuatilia hali za wachezaji ambao
kwa sasa hawako vizuri, akiwemo kiungo Haruna Niyonzima.
Wachezaji
aliokwenda nao Mbeya walikuwa ni makipa; Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barthez’,
mabeki Shadrack Nsajigwa, Juma abdul, Godfrey Taita, Mbuyu Twite, Kevin
Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, David
Luhende, Oscar Joshua na Stefano Mwasyika.
Aliwataja
viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Rashid Gumbo,
Nizar khalfan, Shamte Ally na Simon Msuva, wakati washambuliaji ni Jerry
Tegete, Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi na Hamisi Kiiza, wakati waliobaki
walikuwa ni kipa Said Mohamed, mabeki Ladislaus
Mbogo, Job Ibrahim, viungo Juma Seif ‘Kijiko’, Salum Telela, Omega Seme, Nurdin
Bakari, Idrisa Assega na Issa Ngao wa Yanga B, anayekomazwa kikosi cha kwanza.
0 comments:
Post a Comment