![]() |
Niyonzima na famili yake |
Na Mahmoud Zubeiry
KIUNGO wa
Yanga, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima amerejea Dar es Salaama akiwa mgonjwa
kutoka Mbeya, ambako Jumamosi aliiongoza timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya wenyeji Prisons, ulioisha kwa sare ya bila
kufungana.
Kocha Mkuu
wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet aliiambia BIN ZUBEIRY jana baada ya kutua Dar
es Salaam kwamba wachezaji wote 20 aliokwenda nao Mbeya wamerudi fiti, kasoro
kiungo huyo wa kimataifa wa Rwanda pekee, ndiye ‘anaumwa sana’.
Bado Mtakatifu
Tom ameendelea kusikitikia matokeo ya kuanza na sare katika Ligi Kuu dhidi ya
Prisons, lakini amesema sasa anaelekeza nguvu zake katika mechi ijayo dhidi ya
Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Jumatano.
Mbelgiji huyo,
alilalamikiwa wapinzani wake, Prisons kucheza soka ya kuudhi tangu mwanzo,
ndiyo maana wakapata sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa nyumbani kwao,
Sokoine mjini Mbeya.
Hata hivyo,
Saintfiet alisema amejifunza jambo na anayakubali matokeo hayo na sasa
anajipanga kwa ajili ya mchezo ujao.
“Ilikuwa
mechi ngumu, Prisons walicheza soka ya kuudhi, wakipoteza muda tangu sekunde ya
kwanza,”alisema kocha huyo, ambaye hiyo inakuwa sare yake ya kwanza tangu aanze
kufundisha Yanga Julai mwaka huu, akiwa ameshinda mechi 11 na kufungwa moja.
Mtakatifu
Tom alisema kwamba pamoja na ugumu huo, lakini kipindi cha pili walipata nafasi
za kufunga mabao, ila bahati mbaya walishindwa kuzitumia vema na hana cha
kulamu kwa sababu katika soka wakati mwingine mambo huwa hivyo.
“Kipindi cha
pili tulistahili pointi tatu, Hamisi Kiiza alipiga mashuti matatu mazuri na
Simon Msuva pia moja, lakini kipa wa Prisons akaokoa vizuri sana, hatukucheza
kwa ubora wetu, lakini siwezi kuwalaumu wachezaji wangu, walipambana,
nimesononeka sana,”alisema Mtakatifu alipozungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu
kutoka Mbeya jana.
Yanga Jumamosi
ilianza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kulazimishwa sare ya
bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, huku wapinzani
wao wakubwa katika mbio za taji, Simba na Azam wakiibuka na ushindi.
Simba
iliichapa African Lyon mabao 3-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wafungaji
Emanuel Okwi, Nassor Masoud ‘Chollo’ na Daniel Akuffo, wakati Azam iliichapa
Kagera Sugar 1-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba, mfungaji Abdulhalim Humud.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, kwenye
Uwanja wa Mkwakwani Tanga, bao pekee la kiungo Mkenya, Jerry Santo dakika ya 41
liliipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Mgambo FC.
Uwanja wa
Jamhuri, Morogoro, wenyeji Polisi wamelazimishwa sare ya bila kufungana na
Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu.
Uwanja wa
CCM Kirumba mjini Mwanza, Toto Africans imelazimishwa sare ya 1-1 na JKT
Oljoro, wakati Uwanja wa Chamazi, Mbagala, JKT Ruvu imeifunga Ruvu Shooting
mabao 2-1.
REKODI YA SAINTFIET YANGA
1. Yanga
Vs JKT Ruvu (Kirafiki) 2-0
2. Yanga
Vs Atletico (Burundi, Kagame) 0-2
3. Yanga
Vs Waw Salam (Sudan, Kagame) 7-1
4. Yanga
Vs APR (Rwanda, Kagame) 2-0
5. Yanga
Vs Mafunzo (Z’bar, Kagame) 1-1
(5-3penalti)
6. Yanga
Vs APR (Rwanda, Kagame) 1-0
7. Yanga
Vs Azam (Kagame) 2-0
8. Yanga
Vs African Lyon (Kirafiki) 4-0
9. Yanga
Vs Rayon (Kirafiki, Rwanda) 2-0
10.
Yanga
Vs Polisi (Kirafiiki, Rwanda) 2-1
11.
Yanga
Vs Coastal Union (Kirafiki) 2-1
12.
Yanga
Vs Moro United (Kirafiki) 4-0
13.
Yanga
Vs Prisons (Ligi Kuu) 0-0
0 comments:
Post a Comment