![]() |
Humud katika mechi ya Ngao na Simba, akipambana kutafuta bao dhidi ya beki Amir Maftah na kipa wake, Juma Kaseja |
Na Prince Akbar
PIGO Azam
FC. Kiungo ambaye yuko juu ile mbaya kwa sasa kisoka, Abdulhalim Humud ‘Gaucho’
amerejea na maumivu kutoka Kanda ya Ziwa baada ya kuumia kwenye mechi ya juzi dhidi
ya Toto African, Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara ulioisha kwa sare ya 2-2.
Humud
anaingia kwenye ‘wadi ya wagonjwa’ Chamazi, ambako tayari wamo viungo Salum
Abubakar ‘Sure Boy Jr.’, Hamisi Mcha ‘Vialli’ na mshambuliaji Ibrahim Jeba,
ingawa yeye tatizo lake linaweza kuwa la muda mfupi.
Humud
alifunga katika kila mechi kwenye mbili za Ligi Kuu ilizocheza Azam, dhidi ya
Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba bao pekee la ushindi na jana
katika sare ya 2-2 na Toto alifunga moja na lingine Kipre Herman Tchetche.
Azam FC
inatarajiwa kuwa na mchezo mgumu Jumamosi kwenye Uwanja wa Chamazi, dhidi ya
Mtibwa Sugar, ambayo nayo ineonekana kuwa tishio msimu huu.
Mtibwa iliyoifunga
Yanga 3-0 juzi, ina pointi sawa na Azam, nne kila moja na mechi ya Jumamosi
itakuwa kali kwa sababu kila timu itahitaji ushindi kumuacha mwenzake.
Ikumbukwe
msimu uliopita wa Ligi Kuu, Azam na Mtibwa zilicheza mechi tatu baada ya mbili,
kutokana na mechi moja kuvunjika Chamazi na kurudiwa katika Uwanja wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment