![]() |
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia han Poppe akimkabidhi jezi Paschal Ochieng baada ya kukamilisha usajili. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu'. |
Na Mahmoud Zubeiry
BEKI Mkenya
Paschal Ochieng ana kazi kubwa ya kufanya kujiepusha katika hatari ya kutupiwa
virago Simba SC Desemba mwaka huu, kwani sasa anakabiliwa na wakati mgumu
katika klabu hiyo.
Ochieng
aliyesajiliwa kutoka AFC Leopard ya Kenya, kwa pamoja na beki kutoka Mali,
Komabil Keita waliondolewa kwenye kikosi cha kwanza cha Simba SC na Kocha
Mserbia, Milovan Cirkovick ili warekebishe makosa yao taratibu.
Inaonekana
kama Keita anaanza kuiva na kukaribia kurejea kwenye kikosi cha kwanza, baada
ya jana kupangwa katika kikosi kilichocheza mechi ya kirafiki na Moro United
Uwanja wa Kinesi.
Katika
mchezo huo, bao pekee la mfungaji bora wa mashindano ya Kombe la BancABC,
Christopher Edward dakika ya 43 liliipa ‘Simba Rizevu’ ushindi wa 1-0.
Katika
mchezo huo, Edward ambaye utampenda mazoezini akipangwa timu moja na Mrisho
Ngassa jinsi wanavyoelewana ‘utafikiri walizaliwa pamoja’ angeweza kufunga hata
mabao matatu kama angetumia vema nafasi zote alizopata.
Kikosi cha
Simba jana kilikuwa; Albert Mweta/Hamadi Waziri, Haruna Shamte/Ramadhan Singano
‘Messi’, Komabil Keita, Paul Ngalema, Jonas Mkude, Kiggi Makassy, Haroun Othman,
Christopher Edward, Salim Kinje/Omar Seseme na Felix Sunzu.
Awali ya
hapo, Simba ilicheza mechi ya Ligi Kuu juzi na kuifunga JKT Ruvu mabao 2-0,
wafungaji viungo Amri Kiemba na Haruna Moshi ‘Boban’. Katika mchezo huo wa pili
mfululizo Simba kushinda baada ya awali kuifunga African Lyon 3-0, kikosi
kilikuwa; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Shomary Kapombe,
Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi ‘Boban’, Daniel Akuffo/Ramadhan
Chombo, Mrisho Ngassa/Abdallah Juma na Emanuel Okwi.
0 comments:
Post a Comment