• HABARI MPYA

    Wednesday, September 19, 2012

    ROONEY APONA KIAJABU, ATAKUWEPO MAN U NA GALATASARAY LEO


    Wayne Rooney anaweza kurejea katika kikosi cha Manchester United leo usiku ikimenyana na Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Mshambuliaji huyo alitarajiwa kuwa nje hadi Oktoba baada ya kuumia kwenye mechi dhidi ya Fulham, Agosti 25.
    Crocked: Wayne Rooney missed England's two games through injury
    Wayne Rooney alikosa mechi mbili za England kwa kuwa majeruhi 
    Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, aliumia sana mguu wake wa kulia alipogongwa na Hugo Rodallega wa Fulham, lakini Rooney amepatiwa tiba nzuri na wataalamu wa tiba wa United na amepona kiasi kwamba kwa siku tano amekuwa akifanya mazoezi, limeripoti The Sun.
    Na Rooney anaweza hata kuanzia benchi katika mechi ya ufunguzi ya United ya Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Old Trafford leo.
    Mshambuliaji huyo wa England kwa uhakika zaidi atakuwepo kwenye mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu dhidi ya Liverpool Uwanja wa Anfield. 
    On his way back: Rooney could be a surprise inclusion against Galatasaray
    Rooney anaweza kustaajabisha watu leo kwa kushiriki mechi na Galatasaray

    SOMA ZAIDI: http://www.dailymail.co.uk
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROONEY APONA KIAJABU, ATAKUWEPO MAN U NA GALATASARAY LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top