• HABARI MPYA

    Thursday, September 20, 2012

    SIMBA 'RIZEVU' WAICHAPA MORO UTD 1-0

    Edo Boy

    Na Mahmoud Zubeiry
    SIMBA SC ni baab kubwa- kama hupendi jinyonge. Achana na wanaume wale waliocheza jana na kuitandika JKT Ruvu mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hata wale ambao hawakucheza mechi ya jana ni wa ushindi pia.
    Habari ndiyo hiyo, leo wachezaji ambao hawakushiriki mechi ya jana wamecheza mechi ya kirafiki na timu iliyokuwa Ligi Kuu msimu uliopita tu, Moro United kwenye Uwanja wa Kinesi na kutoa adhabu.
    Mfungaji bora wa mashindano ya Kombe la BancABC, Christopher Edward ndiye alikuwa ‘sterling’ wa kikosi cha wachezaji wa akiba cha Simba leo Kinesi, kwa kufunga bao pekee dakika ya 43.
    Katika mchezo huo, Edward ambaye utampenda mazoezini akipangwa timu moja na Mrisho Ngassa jinsi wanavyoelewana ‘utafikiri walizaliwa pamoja’ angeweza kufunga hata mabao matatu kama angetumia vema nafasi zote alizopata.
    Kikosi cha Simba leo kilikuwa; Albert Mweta/Hamadi Waziri, Haruna Shamte/Ramadhan Singano ‘Messi’, Komabil Keita, Paul Ngalema, Jonas Mkude, Kiggi Makassy, Haroun Othman, Christopher Edward, Salim Kinje/Omar Seseme na Felix Sunzu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA 'RIZEVU' WAICHAPA MORO UTD 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top