Mbuyu Twite akishuka kwenye basi jana Uwanja wa Jamhuri |
Na Mahmoud Zubeiry
YANGA SC wamekumbuka
kitu kinaitwa kambi, baada ya kuanza vibaya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara na hivi unaposoma habari hii, wachezaji wote wa timu hiyo, kasoro majeruhi
wa muda mrefu, Salum Telela leo wamewaachia vitanda wake wazo peke yao na watalala
makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani.
Hatua hiyo
inafuatia kuambulia pointi moja katika mechi mbili za Ligi Kuu, ikitoa sare na
Prisons 0-0 mjini Mbeya Jumamosi na kufungwa 3-0 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro
jana.
Meneja wa
Yanga, Hafidh Saleh ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, wachezaji 30
wameingia kambini leo katika hosteli ya klabu, Jangwani kujiandaa na mchezo wa
Jumamosi dhidi ya JKT Ruvu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hafidh amewataja
wachezaji hao kuwa ni Nizar Khalfan, Athumani
Iddi ‘Chuji’, Shamte Ally Kilalile, Said Rashid Bahanuzi, Haruna Niyonzima
Fadhili, Didier Kavumbagu Fortine, Juma Seif Dion ‘Kijiko’, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’,
Nurdin Bakari Hamad, Said Mohamed, Rashid Omary Gumbo, Juma Jaffar Abdul, Omega
Sunday Seme na Kevin Yondan Patrick.
Wengine ni Jerson
John Tegete, Idrisa Rashid Abdallah, Godfrey Taita Magina, Oscar Joshua Nkulula,
David Charles Luhende, Ibrahim Job Isaac, Ladislaus Mbogo Mahendeka, Ally Mustafa
Mtinge ‘Barthez’, Shadrack Joel Nsajigwa, Hamisi Friday Kiiza, Yaw Koffi Berko,
Stephano Asangalwisye Mwasyika, Mbuyu Twite Banza, Simon Msuva, Frank Domayo na
Issa Ngao.
Wakati Yanga
wanakumbuka kambi baada ya kupoteza pointi tano katika mbio za ubingwa wa Ligi
Kuu, tangu wamerejea kutoka Arusha wiki wiki mbili zilizopita, wapinzani wao wa
jadi, Simba SC wamekuwa kambini hoteli ya Sapphire, Kariakoo, Dar es Salaam.
Kuanza vibaya
kwa Yanga katika Ligi Kuu kumeibua maswali na maoni mengi, kocha akisema
wachezaji wamevimba vichwa na hawajitumi tena, jambo ambalo limeungwa mkono na uongozi
ambao sasa unawaweka chini ya uangalizi maalum wachezaji hao.
0 comments:
Post a Comment