• HABARI MPYA

    Thursday, September 13, 2012

    TAMASHA KUBWA LA MUZIKI HALIJAWAHI KUTOKEA KUFANYIKA LEADERS

    Mwanamuziki mkongwe, Juma Ubao akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa City Sports Lounge, katikati ya Jiji leo kuhusu tamasha la wazi la muziki, litakalofanyika Septemba 28 na 29, viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam. Kuliua kwake ni mwigizaji Jaqcueline Wolper na Mkurugenzi wa EDGE Entertainment, waandaaji wa tamasha hilo, Edwin James Ngere na kushoto ni mdau wa sanaa, Hartman Mbilinyi.

    Mkurugenzi wa EDGE Entertainment, Edwin James Ngere akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa City Sports Lounge, katikati ya Jiji leo wakati wa kutangaza tamasha la wazi la muziki, litakalofanyika Septemba 28 na 29, viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Hamza Kalala ‘Komando’ na Kassim Mapili, wanamuziki wakongwe nchini. Wanaomfuatia Ngere ni mwigizaji Jaqcueline Wolper, mwanamuziki Juma Ubao, mdau wa sanaa, Hartman Mbilinyi, Mratibu wa tamasha, Suzane Migesa na wanamuziki wakongwe, John Kitime na Mafumu Bilal.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAMASHA KUBWA LA MUZIKI HALIJAWAHI KUTOKEA KUFANYIKA LEADERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top