Ofisa Mkuu
wa Biashara wa Zantel, Sajid Khan akimkabidhi jezi, Mkurugenzi wa Michezo,
Leonard Thadeo kwa niaba ya klabu ya African Lyon ya Dar es Salaam, katika
hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kilimanjaro), Dar es Salaam wakati wa kutangaza
kuingia mkataba wa kudhamini klabu hiyo kwa miaka mitatu. Wanaomfuatia Thadeo
ni Meneja Mkuu wa African Lyon, Rahim Kangezi ‘Zamunda’ na Charles Otieno,
Mkurugenzi wa Ufundi wa African Lyon. Kulia kabisa ni mchezaji chipukizi wa
Lyon, Jarufu Magesa, ambaye anapelekwa na klabu hiyo Marekani kusoma na
Kocha Muargentina Pablo Ignacio Velez. Lyon itashuka
dimbani jioni hii kumenyana na Simba SC katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu,
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
|
0 comments:
Post a Comment