BAO la Emmanuel Adebayor dhidi ya wabaguzi wa rangi, Inter Milan limeiwezesha Spurs kutinga Robo Fainali ya Europa League usiku wa jana.
Lilikuwa bao liliwajibu mashabiki wa Inter ambao mwishoni mwa kipindi cha kwanza walimuitia ndizi jukwaani Adebayor wakimfananisha na nyani.
Matokeo ya jumla baada ya mechi zote mbili yanakuwa 4-4, lakini kwa bao la Adebayor jana Spurs ikilala 4-1 San Siro, imefuzu kwa faida ya bao la ugenini, kwani yenyewe awali ilishinda 3-0 London.
VIKOSI...
Inter Milan: S Handanovic, Zanetti, Chivu, Juan, Jonathan/Andrea Ranocchia dk108, Guarin/Alvarez dk71, Cambiasso, Gargano, Kovacic/Benassi dk79, Palacio, Cassano
Benchi: Belec, Pasa, Belloni, Colombi
Kadi ya njano: Juan
Wafungaji wa mabao: Cassano dk20, Palacio dk52, Gallas dk75 (kujifunga), Alvarez dk110
Tottenham: Friedel, Vertonghen, Gallas, Naughton/Caulker dk104, Walker, Parker, Sigurdsson, Livermore/Lennon dk70, Adebayor, Defoe/Holtby dk56, Dembele
Benchi: Lloris, Assou-Ekotto, Huddlestone, Carroll
Booked: Friedel, Livermore, Walker, Holtby, Adebayor
Mfungaji wa bao: Adebayor dk96
Refa: Ivan Bebek (Croatia)
Mahudhurio: 18,241
Emmanuel Adebayor akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia bao Tottenham katika dakika za nyongeza
ZILIZOINGIA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE
Tottenham, Chelsea, Newcastle, Rubin Kazan,Fenerbahce, Lazio, FC Basle, Benfica
Suprs jana ilicheza bila nyota wake Gareth Bale, ambaye alikuwa anatumikia aadhabu ya kadi tatu za njano kuanzia mechi ya kwanza dhidi ya Inter Milan, Aaron Lennon aliyechukua nafasi yake alifanya kazi nzuri ya kupendeza