• HABARI MPYA

    Saturday, March 16, 2013

    AZAM FC: HATUMDHULUMU MTU HAKI ZA TV, TIMU ZOTE ZINALIPWA FUBA LA MAANA

    Himid Mao wa Azam akipambana na mchezaji wa Coastal Union ya Tanga, huku Salum Abubakar 'Sure Boy' akiwa tayari kumsaidia. Azam imekuwa ikionyesha mechi zake zote na kuzilipa timu inazocheza nazo.

    Na Prince Akbar
    UONGOZI wa Azam FC, umesema kwamba katika mkataba wake maalum na kituo cha Televisheni cha Star TV kurusha mechi za timu hiyo, kuna kipengele cha timu zinazocheza nao, kulipwa Sh. Milioni 1 kwa kila mechi.
    Meneja wa Azam FC, Patrick Kahemele ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, timu zote ambazo zimekuwa zikicheza na Azam kwanza, zimekuwa zikiridhia malipo hayo na pili zimekuwa zikilipwa.
    “Leo kuna habari zimetokea, eti Azam inazidhulumu haki ya TV timu inazocheza nazo, hii si kweli, mbaya zaidi imewazungumzia JKT Ruvu, ambao tulipocheza nao, walichukua fedha, na aliyechukua ni Katibu wao,”alisema Kahemele.
    Kahemele alisema katika hali ya kawaida, mechi ambazo hazizihusishi Simba na Yanga dhidi ya Azam ambazo huchezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ambazo hazivutii mashabiki wengi, kuzipa Sh. Milioni 1 klabu hizo dhahiri ni kuzisaidia.
    Kahemele amesema kwamba vyema vyombo vya Habari nchini vikawa mstari wa mbele katika kusaidia maendeleo ya soka nchini na si kukubali kuleta mizengwe ambayo haina tija.
    “Hebu tufikirie jamani, kweli Azam na JKT Ruvu pale Chamazi, kuna timu ambayo inaweza kupata mgawo tu wa mechi hata zaidi ya Sh. 300,000? Hiyo 100,000 yenyewe kwa mbinde.
    Sasa kumpa mtu Sh. Milioni 1 kwa kurusha mechi kwenye TV si kumsaidia jamani? Azam tunaingia gharama zaidi bila kujali hasara kwa sababu tunaangalia mbele, hivyo vyema tukapata sapoti ya vyombo vya habari,”alisema Kahemele. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM FC: HATUMDHULUMU MTU HAKI ZA TV, TIMU ZOTE ZINALIPWA FUBA LA MAANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top