TIMU zote tatu za England zimepangwa tofauti katika Robo Fainali ya Ligi Europa.
Baada ya kufuzu ndani ya dakika 120 dhidi ya Inter Milan, Tottenham imepangwa kumenyana na FC Basel, wakati Chelsea itamenyana na Rubin Kazan na Newcastle itakwana na Benfica.
Kila timu inafurahia kutokutanishwa na Lazio, ambao wanafikiriwa kuwa wagumu, lakini Chelsea itatakiwa kusafiri hadi Urusi kucheza mechi yao ya ugenini.
Mechi za kwanza itachezwa Alhamisi ya Aprili 4, wakati marudiano zitachezwa wiki moja baadaye Aprili 11.
Emmanuel Adebayor akiteleza kufunga bao muhimu dhidi ya Inter Milan
RATIBA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE...
Chelsea v Rubin Kazan
Tottenham v Basel
Fenerbahce v Lazio
Benfica v Newcastle
Mechi za kwanza Aprili 4 na marudiano Aprili 11