• HABARI MPYA

    Tuesday, March 12, 2013

    IPP YAIKUNG'UTA VIBAYA JAMBO LEO, BTL NDIYO YAIFANYA KITU MBAYA ZAIDI CHANGAMOTO KOMBE LA NSSF NETIBOLI NA UHURU YANG'ARA SOKA

    Mchezaji wa akiba wa timu ya Netiboli ya Business Times, Yvonne Cherryl 'Monalisa' akifuatilia mechi kati ya timu yake na Changamoto, michuano ya Kombe la NSSF inayoshirikisha vyombo mbalimbali vya habari nchini jioni ya leo kwenye viwanja vya TCC, Chang'ombe, Dar es Salaam. Business Times ilishinda 64-3 na Mona alifunga sana alipoingia.

    Mshambuliaji wa Uhuru, Said Ambua (kushoto) akimiliki mpira dhidi ya wachezaji wa Mlimani katika michuano ya Kombe la NSSF inayoshirikisha vyombo mbalimbali vya habari nchini jioni hii kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe, Dar es Salaam. Uhuru ilishinda 2-1.

    Mchezaji wa Business Times Limited, Lulu Abeid (kulia) aktumbukiza mpira kwenye kikapu wakati wa mchezo wa Netiboli dhidi yao na Changamoto. BTL ilishinda 64-3. 

    Mchezaji wa Mlimani, Peter Magoda kulia akigombea mpira na mchezaji wa Uhuru

    Hawa Sule wa IPP aliyeruka kuudaka mpira dhidi ya wachezaji wa Jambo Leo. IPP ilishinda 33-4. 

    Hawa Sule akiuficha mpira katika himaya yake

    Somoe Ng'itu wa IPP akimfariji shoga yake, Asha Kigundula wa Jambo Leo baada ya kuwapiga kipigo cha paka jizi la kunyatia jikoni, 33-4.

    Lulu Abeid wa BTL kulia akidaka pasi mbele ya mchezaji wa Changamoto, Maua Magona

    Mchezaji wa BTL, Elizabeth Mbasa akijiandaa kutoa pasi kulia baada ya kumiliki mpira

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: IPP YAIKUNG'UTA VIBAYA JAMBO LEO, BTL NDIYO YAIFANYA KITU MBAYA ZAIDI CHANGAMOTO KOMBE LA NSSF NETIBOLI NA UHURU YANG'ARA SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top