KLABU ya Barnsley imepewa msaada na kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson katika jitihada zao za kuing'oa Manchester City kwenye raundi ya sita ya Kombe la FA leo Jumamosi Uwanja wa Etihad.
Baada ya sare ya 1-1 nyumbani Burnley usiku wa Jumanne, kocha wa Barnsley David Flitcroft aliwapangia wachezaji wake hoteli na kuandaa mazingira ya kufanya mazoezi maeneo ya Manchester katika siku tatu zilizofuata.
Habari njema kwao ni kwamba, Man United ikawakubali kuwafungulia ya Uwanja wao wa mazoezi, Carrington ili klabu hiyo ya Daraja la Kwanza ijifue hapo.
Kumbuka, Man City waliwapa Uwanja wa mazoezi Real Madrid walipokwenda kumenyana na United katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki hii na sasa Mashetani Wekundu wanalipa kisasi.
Kocha David Flitcroft wa Barnsley akiwa mazoezini kwenye Uwanja wa Man United kujiandaa kuing'oa City
Sir Alex Ferguson amewafungulia milango wapinzani wa City Carrington tangu juzi


.png)