KWA namna yoyote mambo yamekuwa yakimuendea vizuri Didier Drogba tangu alipojiunga na Galatasaray.
Lakini Ijumaa usiku gwiji huyo mkali wa mabao, mambo yalimuendea ovyo katika mechi dhidi ya Genclerbirligi.
Alikwenda chini kiulaini kwenye eneo la hatari na ingawa hakulalamika, lakini alizawadiwa penalti.
Didier Drogba akienda chini baada ya kupewa kashikashi kidogo tu
Lakini nyota huyo wa Ivory Coast akakosa penalti
Kwa hasira, Drogba akapiga nyasi eneo ambalo hutengwa mpira wakati wa penalti
Mbaya zaidi mwisho wa mchezo, timu ya Drogba ililala 1-0.
VIDEO: Angalia mambo ya Drogba jana...


.png)