MASHABIKI wa klabu ya Al-Ahly ya Cairo, wamevamia ofisi za Shirikisho la Soka Misri makao makuu na kuzichoma moto kwa hasira za wenzao kuhukumiwa kifo kutokana na vurugu za mwaka jana kwenye Uwanja wa Port Said.
Mapema leo, Korti ya Cairo imethibitisha hukumu ya kifo waliyopewa mashabiki wa soka 21 kutokana na kuhusika na vurugu hizo, ambazo zilisababisha vifo vya watu 74 na wengine 1,000 kujeruhiwa.
Moto pia ulifika hadi kwenye kituo cha Polisi jirani, lakini haijajulikana kwa uhakika kama ni mashabiki wa Al-Ahly waliohusika na tukio hilo.
Mashabiki wa Al-Ahly wakihamaki baada ya hukumu ya kifo kwa wenzao kuidhinishwa leo kutokana na vurugu za Uwanja wa Port Said mwaka jana
Ndani ya Cairo, mashabiki wa Al-Ahly wakichoma moto ofisi za shirikisho
Jamaa akilalamikia uamuzi wa korti leo kuhusu tukio la vurguu kwenye Uwanja wa Port Said mwaka jana. Wengi wa waliohukumiwa kifo ni mashabiki wa Al Masry


.png)