• HABARI MPYA

    Sunday, March 10, 2013

    NIZAR AFANYE NINI MAKOCHA YANGA WAMUELEWE?

    Nizar Khalfan; Shujaa wa Yanga jana

    Na Mahmoud Zubeiry
    NIZAR Khalfan, jana amefunga bao la tano tangu ajiunge na Yanga SC msimu huu akitokea Marekani alikokuwa akicheza soka ya kulipwa.
    Nizar ambaye amekuwa akitokea benchi mara chache, alifunga bao hilo la tano katika mechi yake ya 14, mechi 13 kati ya hizo akitokea benchi zote.
    Tangu wakati wa kocha Mbelgiji, Tom Saintfiet, Nizar Khalfan amekuwa mchezaji ambaye hapewi nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza na mechi nyingi amekuwa akimalizia benchi.
    Desturi hiyo imeendelea hata mbele ya Mholanzi, Ernie Brandts, naye pia hampi nafasi kwenye kikosi cha kwanza kiungo huyo wa kihistoria katika soka ya Tanzania.
    Lakini katika mechi chache ambazo Nizar amekuwa akiingia kutokea benchi, amekuwa akifanya mambo ya maana, kama hafungi basi atatengeneza nafasi za wengine kufunga.
    Jana Nizar aliingia uwanjani dakika ya 64 kuchukua nafasi ya Jerry Tegete na akaifungia Yanga bao dakika ya 78, zikiwa ni dakika 14 tangu avuke mstari wa kuingia uwanjani.
    Aidha, hii inakuwa mechi ya tatu mfululizo, washambuliaji wa Yanga wanashindwa kufunga mabao, kuanzia mechi na Azam FC, Kagera Sugar na jana Toto.
    Katika mechi mbili za awali, Azam na Kagera ambazo Yanga ilishinda 1-0 kila mechi, mabao yalifungwa na kiungo Haruna Niyonzima.  
    Pamoja na Nizar kuonekana mchezaji mwenye msaada katika timu, lakini bado makocha wa timu hiyo hawajashawishika kumuamini kwa aslimia 100. Kwa nini? 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NIZAR AFANYE NINI MAKOCHA YANGA WAMUELEWE? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top