• HABARI MPYA

    Sunday, March 10, 2013

    BREAKING NEWS; SIMBA WAFUNGIWA HOTELINI KWA DENI WAKIJIANDAA KWENDA KUMENYANA NA COASTAL

    Simba SC

    Na Mahmoud Zubeiry
    WACHEZAJI wa Simba SC, wamefungiwa katika hoteli ya Sapphire Court, Kariakoo, Dar es Salaam na kuzuiwa kutoka kwenda Uwanja wa Taifa, kumenyana na Coastal Union kutoana na ukubwa wa deni.
    Mhudumu mmoja wa hoteli hiyo, ameiambia BIN ZUBEIRY mida hii kwamba kuna mgogoro kati ya Simba na Menejimenti ya hoteli na timu imefungiwa hadi deni lilipwe.
    “Deni ni kubwa sana na bosi hayupo, pia Simba wenyewe wana mgogoro kwa sasa, sasa lazima deni lilipwe ndipo timu itoke,”alisema Mhudumu hiyo ambaye aliomba jina lake lisitajwe. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BREAKING NEWS; SIMBA WAFUNGIWA HOTELINI KWA DENI WAKIJIANDAA KWENDA KUMENYANA NA COASTAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top