DROO YA ROBO FAINALI ULAYA...
Malaga v Borussia Dortmund
Real Madrid v Galatasaray
PSG v Barcelona
Bayern Munich v Juventus
(Mechi zitachezwa Aprili 2 na 3 na marudiano Aprili 9 na 10.
IMETOKA DAILY MAIL UK
KIUNGO David Beckham na timu yake PSG watamenyana na Lionel Messi na Barcelona katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wakati Zlatan Ibrahimovic ataikosa mechi ya kwanza kutokana na kutumikia adhabu, Barcelona watakuwa na matumaini ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa marudiano nyumbani Nou Camp.
Katika droo iliyopangwa mjini Nyon, timu mbili zinazopewa nafasi kubwa Real Madrid na Barcelona, zinaonekana kupangiwa timu vibonde, lakini Jose Mourinho atatumai faraja kukutana tena na mshambuliaji wake wa zamani Didier Drogba.
Borussia Dortmund itamenyana na Malaga na vigogo wengine wawili Ulaya, Bayern Munich na Juventus watapambana wenyewe kwa wenyewe Uwanja wa Allianz.
DROO YA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE NAYO HII HAPA...
Mechi ya kwanza - April 4
Chelsea v Rubin Kazan
Tottenham v Basle
Fenerbahce v Lazio
Benfica v Newcastle
Mechi ya marudiano - April 11
Rubin Kazan v Chelsea
Basle v Tottenham
Lazio v Fenerbahce
Newcastle v Benfica
Karibu Leo: David Beckham na PSG watamenyana na Messi na Barcelona yake
Marafiki wanakutana: Kocha wa zamani Chelsea, Jose Mourinho (kushoto) atapambana na mshambuliaji wake wa zamani, Didier Drogba
Mechi za kwanza za Robo Fainali zitachezwa Aprili 2 na 3 na marudiano zitakuwa Aprili 9 na 10, wakati droo ya Nusu Fainali itapangwa Aprili 12.
Taji kubwa: Timu nane zitamenyana sasa kuwania ndoo hii ya thamani kubwa Ulaya
Wanaanzia ugenini: Borussia Dortmund wataifuata Malaga katika mechi ya kwanza
Safari Istanbul: Cristiano Ronaldo atasafiri kumfuata Didier Drogba na Galatasaray yake