• HABARI MPYA

    Tuesday, March 12, 2013

    SIMBA YAMPANGIA NYUMBA SINZA KWA VIMWANA KIPA WAKE NGONGOTI MGANDA

    Abbel Dhaira

    Na Princess Asia
    UONGOZI wa Simba SC, umefanikiwa kuwapatia  nyumba ya kuishi wachezaji wake wa kigeni, kipa Abbel Dhaira na kiungo Mussa Mudde raia wa Uganda, ambao sasa watakuwa wakiishi Sinza, Dar es Salaam eneo maarufu kwa vimwana wakali wenye mitego ya kumtoa nyoka pangni Jijini.
    Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba wakati huo huo, jitihada za kumpatia nyumba na kocha Mfaransa Patrick Liewig zinaendelea.
    “Kwanza nataka niweke sawa, wachezaji hao hawakufukuzwa katika hoteli ya Spice, ni kweli tunadaiwa Spice Hotel, ila hawakufukuzwa, bali kulitokea tatizo la mawasiliano baina yetu,”alisema Mtawala.
    Katibu huyo alisema kwamba kwa kawaida timu inapoingia kambini wachezaji huachia vyumba vya Spice na baada ya kambi wanarudi kwenye hoteli hiyo.
    “Lakini hatukuwa na mawasilianio ya mapema na uongozi wa Spice juu ya wachezaji hao kurejea hapo, hivyo walipofika, wakakuta vyumba vimejaa, ndipo ikabidi waende kutafuta malazi sehemu nyingine,”alisema Mtawala. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA YAMPANGIA NYUMBA SINZA KWA VIMWANA KIPA WAKE NGONGOTI MGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top