• HABARI MPYA

    Tuesday, March 12, 2013

    UCHAGUZI TAFCA KUFANYIKA MOROGORO


    Na Boniface Wambura
    UCHAGUZI wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Soka Tanzania (TAFCA) utafanyika Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) mjini Dodoma ambapo wajumbe wanatakiwa kuripoti siku moja kabla ya uchaguzi.
    Wagombea waliopitishwa kuwania uongozi na Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA chini ya uenyekiti wa Ramadhan Mambosasa ni Oscar Don Koroso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti) na Katibu (Michael Bundala).
    Wengine ni Gabriel Gunda (Katibu Msaidizi), Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania- TFF (Wilfred Kidao) wakati wagombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Jemedali Saidi, George Komba na Magoma Rugora.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: UCHAGUZI TAFCA KUFANYIKA MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top