ROBIN van Persie ndiyo mchezaji maarufu zaidi kwenye Ligi Kuu ya England, hii ni kutokana na idadi ya jezi zilizouzwa.
Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Uholanzi, ameruka mpaka kukamata namba moja kwenye mauzo ya jezi akichukua nafasi ya mshambuliaji mwenzake wa Manchester United, Wayne Rooney.
Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal, ametawala soko la jezi huku asilimia 25.4 ya ya vifaa vyote vya michezo ambavyo vimeuzwa ni vile vyenye jina la V.Persie 20.
Unaweza kuvaa jezi yake: Jezi namba 20 ya Robin Van Persie, ndiyo inauzwa zaidi England
Kiwango: Uwanjani pia mambo siyo mabaya kwake amefunga mabao 19, na kuweka Man United kileleni mwa Ligi Kuu ya England
JEZI 10 BORA KWA MAUZO UINGEREZA
1) Van Persie (20) – 25.4%
2) Gerrard (8) – 8.2%
3) Rooney (10) – 6%
4) Kagawa (26) 5.8%
5) Suarez (7) – 3.6%
6) Hazard (17) – 3.1%
7) Scholes (22) – 2.7%
8) Torres (9) – 2.5%
9) Kun Aguero (16) – 2.2%
10) Podolski (9) – 2.1%
Uchunguzi wa kitbag.com
Van Persie ambaye amesajili kwa pauni milioni 24, Sir Alex Ferguson, anaonekana kulamba dume kutokana na usajili huo kwa sababu tayari mshambuliaji huyo ameshafunga mabao 19 kwenye Ligi Kuu, na jezi yake pia inauzika sana.
Usajili mwingine uliofanywa na klabu hiyo wakati wa Kiangazi, Mjapan Shinji Kagawa, anaonekana kuwa muhimu kibiashara kutokana na kuingiza asilimia 5,8 ya mauzo yote ya jezi. Kupanda kwa kiwango cha Kagawa ni dalili tosha kwamba mauzo ya jezi zake yatapanda zaidi.
Lakini siyo kila kitu kinaenda sawa Old Trafford, wakati huu ambao Wayne Rooney yuko kwenye wakati mgumu kutokana na mafanikio ya washikaji zake.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtandao wa kitbag.com, mshambuliaji wa huyo kimataifa wa England ameshuka sana msimu huu, akianguka hadi kwenye nafasi ya tatu, mauzo ya jezi yake yakipungua kwa asilimia 2.4, wakati Ryan Giggs na Javier Hernandez wakiporomoka kutoka kwenye 10 bora.
“Robin van Persie ni mchezaji wa hadhi ya dunia, kiwango chake kimemfanya awe mchezaji maarufu zaidi kwenye Ligi Kuu ya England,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa kitbag.com, Andy Anson.
Yuko juu, Mario: Jezi ya Balotelli ndiyo inaongoza kwa mauzo kwenye klabu ya Manchester City msimu huu – ameondoka Man City Januari
Mauzo United: Kagawa na Rooney nao pia hawako nyuma katika mauzo ya jezi
“Baada ya kuhamia Manchester United, siyo jambo la kushangaza kuona mashabiki wa soka wa Uingereza wakimuunga mkono kwa kununua jezi yake.
“Kwa kuangalia majibu, ni jambao la kujivunia kuona wachezaji wawili wa Uingereza wakiwa kwenye tatu bora, inaonyesha kwamba mashabiki wanawakubali wachezaji wa nyumbani.”
Jezi za nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard zimepanda hadi kufikia hatua ya nafasi ya pili, huku akiongoza mauzo ya jezi kwenye soko la Amerika akiwa na asilimia 10 ya mauzo yote huko.
Pia yuko mbele ya mfungaji bora wa Liverpool, Luis Suarez, baada ya kutawala soko la mauzo ya jkezi ya Liverpool akiwa na asilimia 52.6, kulinganisha na asilimia 23 za Suarez.
Mjerumani zaidi ya Mwingereza? Mashabiki wa Arsenal wamenunua jezi nyingi zaidi za Lukas Podolski kuliko kwa Jack Wilshere.
Mjerumani anamzidi Muingereza? Mashabiki wa Arsenal wananunua zaidi jezi za Lukas Podolski kuliko za Jack Wilshere
Bado namba 1: Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard (kushoto) bado yuko juu ya Luis Suarez kwa mauzo kwenye klabu hiyo.
WAUZAJI BORA WA 'BIG FIVE'
MANCHESTER UNITED:
Robin van Persie (20) asilimia 48
Wayne Rooney (10) asilimia 11.4
Shinji Kagawa (26) asilimia 11.1
MANCHESTER CITY:
Sergio 'Kun' Aguero (16) asilimia 24
Mario Balotelli (45) asilimia 13.0
David Silva (21) asilimia 8.4
CHELSEA:
Eden Hazard (17) asilimia 23.0
Fernando Torres (9) asilimia 18.7
Juan Mata (10) asilimia 14.1
ARSENAL:
Lukas Podolski (9) asilimia 18.4
Jack Wilshere (10) asilimia 17.6
Alex Oxlade-Chamberlain (15) asilimia 11.0
LIVERPOOL:
Steven Gerrard (8) asilimia 52.6
Luis Suarez (7) asilimia 23
Daniel Agger (5) asilimia 7
Sehemu kubwa ya mashabiki wa Manchester City, wamepoteza fedha zao msimu huu.
Wamenunua jezi nyingi za mshambuliaji wao aliyeihama klabu hiyo siku za karibuni, Mario Balotelli anashikilia nafasi ya pili katika mauzo ya jezi ya klabu hiyo, jezi namba 45 ya Balotelli imeuzwa kwa asilimia 13.0
Mashabiki Arsenal, hawajaona hatari kumchagua Mjerumani zaidi ya Mwingereza, Lukas Podolski ameingia kwenye 10 ya mauzo ya jezi huku akiongoza mauzo ya jezi Arsenal akiwa mbele ya Jack Wilshere.
Gwiji wa Chelsea Frank Lampard ameshindwa hata kuingia kwenye tatu bora ya mauzo ya jezi kwenye klabu yake.
Mtu pekee ambaye hajuuza jezi hata moja ni Nicklas Bendtner.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark ameshindwa kuuza jezi hata moja kwenye klabu yake ya Juventus tangu ahamie, jezi namba ya Bendtner, haina soko kabisa Turin.
Staa huyo aliye kwa mkopo kwenye Juventus alibadilisha jezi namba yake akiwa Arsenal kutoka namba 26 hadi 52 kwa sababu alikuwa amesaini mkataba wa kumuingizia pauni 52,000 kwa wiki, kitu ambacho alikanusha kwenye mahojiano na Sportsmail.
Ni wapi staa aliye kwenye fomu kubwa kwa sasa kwenye ligi alipo linapokuja suala la mauzo ya jezi, Gareth Bale yuko wapi?Kitbag hawakupata hata takwimu zake.
Maarufu zaidi: Eden Hazard ndio anaongoza mauzo ya jei Chelsea, - Frank Lampard hayupo hata tatu bora.
Bure kabisa: Juventus hawajauza kabisa jezi za Nicklas Bendtner (kulia) tangu ajiunge nao.
Hayupo popote: Hakuna takwimu za mauzo ya jezi namba 11 ya Bale.


.png)