IMEWEKWA JUNI 14, 2013 SAA 11:00 JIONI
MWANASOKA wa zamani wa Tanzania, Abdallah Msamba amezikwa mchana wa leo makaburi ya Magomeni Makuti, Dar es Salaam katika mazishi yaliyohudhuriwa na mamia ya wachezaji mbalimbali, wengi wakiwa wastaafu na haswa aliocheza nao enzi zake.
Shrikisho la Soka Tanzania (TFF) liliwakilishwa na Mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji, Ahmed Mgoyi, wakati sehemu kubwa ya walioshiriki walikuwa ni wachezaji tu.
TFF imesema imepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mchezaji huyo wa zamani wa timu za Pan Africans, Simba na Taifa Stars, Abdallah Msamba kilichotokea juzi usiku (Juni 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
TFF imesema msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Msamba akiwa mchezaji, na baadaye kocha wa timu kadhaa alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea na kufundisha ikiwemo Villa Squad, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
Imesema inatoa pole kwa familia ya marehemu Msamba, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA) na klabu ya Villa Squad na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
 |
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu Abdallah Msamba |
 |
Wakiwa kwenye kaburi la marehemu baada ya mazishi. Hapa mkakati ni kulijengea. |
 |
Boniface Pawasa kushoto akizungumza jambo baada ya mazishi |
 |
Ally Mayay akizungumza jambo baada ya mazishi |
 |
Kulia Iddi Moshi na kushoto Twaha Hamidu 'Noriega' |
 |
Mabeki wa zamani wa Simba SC, Amri Said na Adolph Kondo kushoto |
 |
Mdau maarufu wa soka nchini na Meneja wa zamani wa Yanga SC, Hamisi Ambari kushoto akiwa na wachezaji mbalimbali |
 |
Wachezaji mbalimbali msibani |
 |
Wachezaji mbalimbali wa zamani msibani |
 |
Kocha wa Simba Jamhuri Kihwelo akizungumza baada ya mazishi. Kushoto kwake ni George Lucas na nyuma ni Iddi Selemani na John Mwansasu |