IMEWEKWA JUNI 8, 2013 SAA 4:25 USIKU
KLABU ya Chelsea inajipanga kuiingia tena Napoli na ofa kubwa kwa ajili ya mshambuliaji Edinson Cavani baada ya ofa yao ya awali kukataliwa jana Ijumaa.
Mazungumzo baina ya klabu hizo mbili yanaendelea na klabu hiyo ya Stamford Bridge ipo tayari kupanda dau.
Dau la Pauni Milioni 40 lililotolewa pamoja na kipa Thibaut Courtois ambaye yupo kwa mkopo Atletico Madrid msimu uliopita limekataliwa.
Mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani (katikati) anatakiwa na Cheslea
Lakini Rais wa Napoli, Aurelio de Laurentiis aliwakatalia Chelsea na kuwaambia hawatamuuza Cavani kwa dau la chini ya Pauni Milioni 53.
Mazungumzo yataendelea wikiendi hii na kuna dalili Chelsea itamtumia Fernando Torres kama sehemu ya mpango wa kumnasa mpachika mabao huyo wa kimataifa wa Uruguay.