• HABARI MPYA

    Wednesday, June 12, 2013

    KAPTENI HANS POPPE ALA 'ZA USO' TUNISIA, SASA AWAPA MUDA ETOILE HADI SEPTEMBA VINGINEVYO KESI INAHAMIA FIFA


    Za uso; Kapteni wa zamani JWTZ, Hans Poppe akiwa makao makuu ya Etoile du Sahel leo. Deni  la Okwi ameahidiwa kulipwa Septemba mwaka huu.
    Na Mahmoud Zubeiry, Marekech, IMEWEKWA JUNI 12, 2013 SAA 10:50 JIONI
    KLABU ya Etoile du Sahel ya Tunisia imeahidi kulipa dola za Kimarekani 300, inazodaiwa na klabu ya Simba SC YA Dar es Salaam kutokana na mauzo ya mshambuliaji Mganda Emmanuel Anord Okwi ifikapo Septemba mwaka huu, kwa kuwa hivi sasa inakabiliwa na hali ya ngumu ya kifedha.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY kutoka Tunis, Tunisia mida hii, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba sasa wanarejea Dar es Salaam kusikilizia ahadi hiyo mpya baada ya klabu hiyo ya Tunisia kushindwa kulipa fedha hizo tangu wamnunue mchezaji huyo Januari mwaka huu.
    “Ni kweli hawa jamaa pamoja na klabu nyingine zote za Tunisia wanakabiliwa na tatizo la kifedha, kwa sababu wanacheza mechi hakuna mashabiki uwanjani. Hawa jamaa walitegemea kutulipa kutokana na dili yao ya udhamini, ambayo waliipoteza mara tu walipomsaini Okwi,”alisema Hans Poppe.
    Jengo zuri, hawana fedha; Makao makuu ya Etoile, Hans Poppe huyo!

    Hans Poppe alisema sasa Etoile wameahidi kuilipa Simba SC baada ya kupata fedha zao za mgawo kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Septemba mwaka huu.    
    Poppe aliunganisha safari Jumapili kwenda Tunisia, akitokea Marakech, ambako alikwenda kuisapoti timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa ikimenyana na wenyeji Morocco Jumamosi na kufungwa 2-1 kuda fedha hizo.
    Poppe, ambaye Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), aliungana na Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala aliyetangulia mjini Tunis siku moja kabla akitokea Dar es Salaam.
    Wakati anaondoka Marakech, Poppe alisema; “Tumekuwa tukiwaandikia sana barua Etoile lakini hawajibu, sasa tumeamua kufuata kanuni, tunaanzia kwenda kushitaki kwenye FA yao, baada ya hapo tunakwenda FIFA,”.
    Okwi aliuzwa katika klabu hiyo Januari mwaka huu na hadi sasa Simba SC imekuwa ikisotea fedha za muazo yake.   
    Poppe alisema iwapo ikifika Septemba fedha hizo hazijalipwa watafungua kesi Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KAPTENI HANS POPPE ALA 'ZA USO' TUNISIA, SASA AWAPA MUDA ETOILE HADI SEPTEMBA VINGINEVYO KESI INAHAMIA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top