IMEWEKWA JUNI 16, 2013 SAA 6:00 MCHANA
MCHEZAJI wa pili wa Newcastle amepata ushauri mzuri kuhusu jezi za wadhamini, kampuni ya mikopo ya Wonga.
Cheick Tiote anatarajiwa kukutana na uongozi wa klabu wiki ijayo akitoka Tanzania, ambako amekuja kuichezea nchi yake, Ivory Coast dhidi ya wenyeji mechi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani.
Mshambuliaji Papiss Cisse tayari ameelezea msimamo wake wa kutokuwa tayari kuvaa jezi zenye tangazo la Wonga, lakini yeye wachezaji wenzake Waislamu, Tiote, Massaido Haidara, Hatem Ben Arfa na Moussa Sissoko walipozi kupiga pichazenye nembo ya wonga.com Aprili mwaka huu kuipromoti kampuni hiyo.
Hajakubali: Cheick Tiote atakutana na uongozi wa Newcastle juu ya jezi mpya za wadhamini, Wonga
Cisse na Tiote hawakuwa wanajua asili ya biashara ya Wonga wakati wanapiga picha hizo kwa sababu klabu haikuwaambia ukweli.
Sheria ya Kiislamu inakataza kula riba na hiyo ndiyo biashara ya Wonga.
Newcastle imetoa picha ya Steven Taylor pekee akiwa na nembo mpya ya Wonga — lakini picha za wachezaji wengine zinatarajiwa kutolewa hivi karibuni.
Newcastle ilitangaza Mkataba wa miaka minne wenye thamani ya Pauni milioni 24 na Wonga, Oktoba mwaka jana na timu itavaa jezi lenye jina ya kampuni yao msimu ujao.
Tiote alizungumza na mwakilishi wake katika masuala ya kisheria wiki iliyopita na anatarajiwa kukutana na Mtendaji Mkuu wa Newcastle, Derek Llambias.
Hataki: Papiss Cisse anaweza kulazimika kuondoka Newcastle katika mgogoro wa nembo ya wadhamini kwenye jezi
Cisse, aliyesajiliwa kutoka Freiburg ya Ujerumani kwa Pauni Milioni 8 mwaka 2011, anaweza kuuzwa iwapo hatakubali kuvaa nembo ya Wonga.
Mwonekano mpya: Steven Taylor akiwa na jezi yenye nembo ya Wonga ambayo watavaa Newcastle ugenini msimu ujao