• HABARI MPYA

    Friday, May 16, 2014

    HATARI, KIPA WA ZAMANI ENGLAND DAVID JAMES ATANGAZA KUFILISIKA LICHA YA KUVUNA MAMILIONI KIBAO WAKATI ANACHEZA

    KIPA wa zamani wa England, David James amesema amefilisika.
    James aliingiza kiasi cha Pauni Milioni 20 wakati wake anacheza akiwa na klabu za Manchester City, lakini kwa mujibu wa The Sun, mambo yalianza kwenda combo baada ya kutengana na mkewe Tanya mwaka 2005.
    James aliichezea England mechi 53 na pia amechezea klabu za Aston Villa, West Ham na Portsmouth. Alitwaa Kombe la Ligi akiwa na Liverpool mwaka 1995 na Kombe la FA akiwa na Pompey mwaka 2008.
    Majukumu ya kitaifa: David James ameichezea mechi 53 England kati ya mwaka 1997 na 2010
    Highlight: James was part of the Portsmouth side that won the FA Cup in 2008
    Mataji: James alikuwamo kwenye kikosi cha Portsmouth kilichotwaa Kombe la FA mwaka 2008
    Wise words: James (right) now works as a football pundit for BT Sport
    Muuza maneno: James (kulia) kwa sasa ni mchambuzi wa BT Sport

    UHAMISHO WA JAMES

    1992 Liverpool Pauni Milioni 1.25
    1999 Aston Villa Pauni Milioni 1.8
    2001 West Ham Pauni Milioni 3.5
    2004 Manchester City Pauni Milioni 2
    2006 Portsmouth Pauni Milioni 1
    James amewasilisha taarifa ya kufilisika mahakama ya Hertford County Court Ijumaa iliyopita.
    Taarifa hizo zinasema kipa huyo mwenye umri wa miaka 43, ambaye amekuwa akifanya kazi za uchambuzi BT Sport na kutangaza bidhaa za Armani msimu huu, anaweza kukwamuliwa ndani ya mwaka mmoja.
    Kutengana na mkewe Tanya inaaminika kumemgharibu zaidi ya Pauni Milioni 3 katika mali zake. Wawili hap wanamiliki pamoja majengo saba, na mali za James ilikuwa zinaaminika kuwa na thamani ya Pauni Milioni 6 hadi mwaka 2005.
    James alitengana na mkewe baada ya kurudiana na mpenzi wake wa tangu shule, Amanda Salmon, ambaye aliwasiliana nays tena kupitia mtandao wa kijamii, ujulikanao kara Friends Reunited (Marafiki wanungana tena).
    Kipa huyo wa zamani wa Liverpool atapiga kazi kesho BT Sport wajati wa fainali ya Kombe la FA baina ya Arsenal na Hull.

    WASIFU WA DAVID

    David James shares a joke on BT Sport
    Kuzaliwa: Agosti 1, 1970 (Miaka 43)
    Urefu: Futi 6 na inchi 4.5
    Nafasi: Kipa
    Klabu alizochezea: Watford, Liverpool, Aston Villa, West Ham, Manchester City, Portsmouth, Bristol City, Bournemouth
    idadi ya mechi za klabu: 805
    Mechi za kimataifa: 53 England
    Mataji: Kombe la Ligi (1994-95), 
    Kombe la FA (2007-08)
    Kazi ya sasa: Mchambuzi wa BT Sport
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HATARI, KIPA WA ZAMANI ENGLAND DAVID JAMES ATANGAZA KUFILISIKA LICHA YA KUVUNA MAMILIONI KIBAO WAKATI ANACHEZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top