KLABU ya Azam FC imemtambulisha kiungo Himid Mao Mkami (32) kuwa mchezaji wake mpya kwa mkataba wa mwaka mmoja hadi mwaka 2026 akitokea Ghazl El Mahallaya Misri.
Mao 'Ninja' kwa Azam FC ni anarejea nyumbani, klabu iliyomkuza kuanzia ngazi ya akasemi mwaka 2007 hadi alipopandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2008 na akacheza hadi 2018 alipokwenda Misri.
Nchini Misri amechezea klabu za Petrojet (2018–2019), ENPPI (2019–2021) na Ghazl El Mahalla aliyojiunga nayo mwaka 2021.
Mao ni mwanasoka mzoefu anayeweza kucheza nafasi za kiungo na beki wa pembeni ambaye amekulia kwenye misingi halisi ya soka akicheza timu zote za Taifa, kuanzia za vijana chini ya umri wa miaka 15, U-17, U- 20 na U-23 na amekuwa mchezaji wa timu ya wakubwa ya taifa ta
ngu mwaka 2013 akicheza jumla ya mechi 61 na kufunga mabao mawili.
Anakuwa mchezaji mpya wan ne kutambulishwa Azam FC baada ya kipa Aishi Manula kutoka Simba SC, beki Lameck Lawi kutoka Coastal Union na mshambuliaji Muhsin Makame kutoka Zed FC ya Misri.
0 comments:
Post a Comment