• HABARI MPYA

    Thursday, July 10, 2025

    PSG WATINGA FAINALI KOMBE LA DUNIA BAADA YA KUITANDIKA REAL MADRID 4-0


    TIMU ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa imeendelea kudhihirisha umwamba wake kwa wapinzani wake wa Ulaya baada ya usiku wa Jumatano kufanikiwa kuingia Fainali ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA kufuatia ushindi wa mabao 4–0 dhidi ya Real Madrid ya Hispania Uwanja wa MetLife, East Rutherford, Bergen County, New Jersey, Marekani.
    Mabao ya  Paris Saint-Germain ‘Les Parisiens’ (Wana Paris) yamefungwa na kiungo Mspaniola, Fabián Ruiz Pena dakika ya sita na 24 na washambuliaji Mfaransa Masour Ousmane Dembélé anayezaliwa na mama Mmauritania mwenye asilia ya Senegal na baba kutoka Mali dakika ya tisa na Mren

    o, Gonçalo Matias Ramos dakika ya  87.
    Sasa mabingwa hao wa Ulaya, PSG watakutana na Chelsea katika Fainali Julai 13 hapo hapo Uwanja wa MetLife.
    Ikumbukwe Chelsea iliitoa Fluminense ya Brazil kwa kuichapa mabao 2-0 mabao ya mshambuliaji Mbrazil, João Pedro dakika ya 18 na 56 hapo hapo Uwanja wa MetLife.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PSG WATINGA FAINALI KOMBE LA DUNIA BAADA YA KUITANDIKA REAL MADRID 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top